UCHUNGUZI MAUAJI YA KIMBARI NCHINI RWANDA UMEKAMILIKA

Majaji wa Ufaransa wamemaliza upelelezi juu ya shambulio la kombora ambalo lilisababisha kuanza kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.

Kagame
Image captionRais wa Rwanda,Paul Kagame
Ofisi ya mwendesha mashitaka sasa wataamua ikiwa waipeleke kesi mbele ya mahakama ambapo Majaji wamewalaumu wapiganaji walioongozwa na rais wa sasa wa Rwanda Paul Kagame kwa kuilenga na kuiangusha ndege iliyokuwa imembeba rais wa wakati huo wa taifa hilo Juvenal Habyarimana.
Rwanda nayo inawalaumu Ufaransa kwa kushiriki kupanga mauaji ya kimbari huku Upelelezi ukisababisha sintofahamu kati ya mataifa haya mawili kiasi cha Rwanda kuvunja uhusiano wa kidplomasia na ufaransa mwaka 2006.
Hata hivyo Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ulirejeshwa miaka mitatu iliyopita.
Chanzo:bbc

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA