BUNDI GANI AMEENDELEA KUTANDA KUHUSIANA NA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS?TUMEPOROMOKA TENA VIWANGO VYA FIFA MPAKA NAFASI YA 147 KUTOKA 142


Taifa Stars
Tanzania imezidi kudidimia katika viwango vya soka duniani baada ya kushuka kwa nafasi 5 zaidi kwenye viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa mwezi Novemba.
Kupitia taarifa iliyotolewa ljana na Shirikisho la soka duniani FIFA inaonyesha Tanzania inashika nafasi ya 147 kutoka  142 mwezi Oktoba ikiwa imeporomoka kwa nafasi tano kutoka juu.
Kwa Uganda wa Afrika Mashariki na Kati,Uganda imeendelea kuongoza ikiwa inashika nafasi ya 75 duniani huku Senegal ikiwa inaongoza kwa Afrika nzima ikiwa inashika nafasi ya 23 kwenye viwango hivyo vya FIFA.
Kwa upande wa 10 bora,Ujerumani imeendelea kuongoza ikifuatiwa na Brazil,Ureno,Argentina,Ubelgiji,Hispania,Poland, Uswisi,Ufaransa na Chile.
Tanzania ilifanya vibaya kwenye michuano ya CECAFA nchini Kenya mapema mwezi huu pia kwa mwezi Novemba ilipata sare ya 1-1 dhidi ya Benin.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA