MAREKANI KUUTAMBUA JERUSALEM KUWA MJI MKUU WA ISRAEL UN WAPIGA KURA KUPINGA

n
Image captionUmoja wa mataifa kupinga maamuzi ya Trump
Mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa umepiga Kura ya kutoyatambua maamuzi ya Marekani ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Makubaliano hayo ya mkutano wa umoja wa mataifa yamefikiwa pamoja na vitisho vya Rais wa Marekani Donald Trump aliyetishia kuzikatia msaada wa kifedha nchi zote zitakazopinga msimamo wake.
Mataifa 120 wameyapigiakura maazimio,baadhi ya mataifa hayo yakiwamo washirika wa karibu wa marekani yaani Japan, Uingereza na Ujerumani yamepiga kura.
Canada na Mexico ni moja ya mataifa thelathini na tano ambayo hayakuhudhuria mkutano huo na Wapalestina wameiita hatua ya Umoja wa mataifa kuwa ni ushindi wa Palestina ingawa Israel imeyakataa matokeo.
Kabla ya kura,balozi wa marekani katika umoja wa mataifa,Bi Nikki Haley alionya kuwa Marekani haitasahau au kusamehe pale nchi zilizoipinga Marekani zitakapokuja kuomba misaada.
Chanzo:bbc

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA