MTOTO WA KAMANDA MTAAFU SULEIMAN KOVA AMEHUKUMIWA JELA MWAKA MMOJA MKOANI KATAVI KWA UTAPELI,ALIJITAMBULISHA NI MWAKILISHI WA STAR TV MKOANI KATAVI

MAHAKAMA ya mwanzo wilayani Mpanda mkoani Katavi imemuhukumu aliyekuwa akijitambulisha kuwa ni mwakilishi wa  televisheni ya Star Tv mkoani Katavi pia  mtoto wa  Kamanda mstaafu wa Jeshi la polisi  Sulemani Kova anaejulikana kwa  jina la  Gerald  Kova mkazi wa mkoa wa  Mwanza kifungo cha mwaka   mmoja  jela kwa kosa la uapateli.
Hukumu hiyo ilitolewa na hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Marko  Pagyo  baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na  upande wa  mashtaka.
Awali mwendesha mashtaka wa jeshi  la  Polisi Wp Salma alidai Mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo februari  8 mwaka huu katika   eneo la hotel ya Madina katika Manispaa ya Mpanda.
Alidai  kuwa  mshitakiwa  huyo alijipatia kwa  njia ya udanganyifu  Kamera  moja  aina  ya  Canoni yenye thamani ya shilingi 3,500,000 pia computer aina ya  Laptop pamoja na stendi ya Kamera ya video  mali ya Elias Mlugala.
Alisema mtuhumiwa  baada ya  kujipatia  mali  hizo kwa  njia ya   udanganyifu alitoroka wilayani Mpanda  na kutokomea  kusikojulikana.
Alisema vitu alivyotapeli ni camera aina ya Nikon  D 7,200 mali  ya  Chama  cha  Wandishi wa  habari mkoani Katavi yenye  thamani ya  shilingi 4,900.000.
Mwendesha  mashitaka  huyo aliiambia mahakama hiyo kuwa mshitakiwa  baada  ya  kutokomea  kusikojulikana mpaka mwezi Agosti mwaka huu alipokamatwa  Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga akijitambulisha kwa jina  la Crispin  Masawe,alikamatwa baada ya  kufanya amefanya  utapeli mwingine na kujipatia  Lap top  moja ya  mwandishi wa  habari.
Alidai baada ya  kukamatwa    alifikishwa mahakama ya mwanzo  ya Kahama  na  kuhukumiwa  kifungo cha  miezi  mitatu  au  kulipa  faini ya shilingi 100,000  hata  hivyo  hakuweza kulipa na  kwenda gerezani kutumikia kifungo.
Mwendesha  mashta alieleza  ndipo waandishi wa habari wa mkoani katavi  Elias  na   Kibada waliotapeliwa na mtuhumiwa huyo walipopata taarifa  ya kituo cha  polisi cha  Mpanda ya mtuhumiwa  wao  kuhukumiwa   kifungo hicho walianza kufuatilia.
Walifanya utaratibu na  kwenda Kahama na kumlipia  faini na  kumtoa  gerezani kisha akawa  chini ya ulinzi wa  polisi na kusafirishwa  hadi  Mpanda  na  alipofikishwa alionesha vifaa vyote, alivyomuuzia   mfanyabiashara  mmoja wa majimoto wilayani  Mlele mkoani Katavi.
Mshitakiwa Gerald  Kova  katika  utetezi wake kabla ya kusomewa  hukumu  aliiomba  mahakama  imwachie  huru kwa  kile alichodai  kuwa  anakunywa  dawa za  kufubaza makali ya ukimwi ARVs na ana matatizo ya ugonjwa wa  sikoseli pia  mama  yake  mzazi ni  mgonywa  na   anamtegemea  yeye.
Baada  ya  utetezi huo   hakimu  Paragyo  alisoma hukumu  na  kuamuru mshitakiwa  atumikie  kifungo cha mwaka  mmoja jela  na pindi atakapo toka gerezani  atatakiwa  kulipa shilingi 800,000.
Mshitakiwa  huyo   anatarajiwa  kufikishwa tena mahakamani kwa ajiri ya kesi ya  pili ya kuiba kamera aina ya Nicon  mali ya  Chama  cha waandishi wa habari ambapo kesi  hiyo   itasikilizwa.
Hukumu hiyo imtolewa juzi

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA