MAMBO YAMECHACHA NCHINI ZIMBABWE,JESHI LADHIBITI KITUO CHA UTANGAZAJI CHA TAIFA

Mkuu wa jeshi la Zimbabwe Constantino Chiwenga alitahadharisha uwezekano wa jeshi kuchukua nchi
Jeshi nchini Zimbabwe limekidhibiti kituo cha utangazaji cha shirika la habari la taifa hilo ZBC ambapo Sauti za milipuko mikubwa zimesikika mji mkuu wa Zimbabwe Harare.
Wanajeshi wakiwa na silaha nzito wameoneakana wakirandaranda mjini Harare
Rais Robert Mgabe akiwa na mkewe Bi.Grace Mugabe 
Hali hiyo ya wasi wasi wa lolote imetanda nchini humo kuweza kuweza kutokea ambapo wasiwasi huo ulianza jana jioni ambapo wanajeshi wakiwa na silaha walionekana wakijipanga katika maeneo kadhaa pamoja na kuzingira ofisi za shirika la utangazaji la Zimbabwe ZBC.
Hata hivyo taarifa zinasema wafanyakazi wa shirika la utangazaji ZBC,wameambiwa na wanajeshi hao wasiwe na wasiwasi kwamba uwepo wa vikosi hivyo ni kwa lengo la kulinda eneo hilo.
Milipuko mizito imeendelea kusikika pia huku Magari ya wanajeshi waliojihami kwa silaha yakionekana maeneo ya mjini Harare.
Chama tawala nchini Zimbabwe kimemtuhumu mkuu wa majeshi Constantino Chiwenga kwa hatua yake ya madai kuwa jeshi lipo tayari kuingilia mzozo huo wa kisiasa kwa lengo la kulinda wapigania uhuru wa taifa hilo.
Marekani imesema inafuatilia kwa karibu hali ya Zimbabwe na kutoa rai pande zote kutatua mzozo huo kwa njia ya amani ambapo mpaka sasa hakuna kauli yoyote iliyotolewa na Rais Robert Mugabe kutokana na hali ya sasa nchini mwake.
Naye Balozi wa Marekani nchini Zimbabwe kupitia ukurasa wake wa Tiwtter amesema leo watasitisha shughuli za kiofisi ubalozini hapo kutokana na hali ya sasa mjini Harare.
Balozi wa Zimbabwe nchini Afrika Kusini Isack Moyo ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa serikali ipo imara katika jambo hilo na kuzuia uwezekano wowote wa kufanyika kwa mapinduzi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA