MASHA AMEJIVUA UANACHAMA CHADEMA

Aliyekuwa mwanachama CCM, ambaye baadaye alihamia Chadema,Lawrance Masha amejivua uanachama katika chama hicho akidai  upinzani wa sasa umeridhika na hali ya kuendelea  kuwa wakosoaji ili kukisaidia chama tawala kujirekebisha.
Masha ameeleza hayo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana Jumanne Novemba 14.
Masha ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, katika Serikali ya awamu nne, amesema upinzani hauwezi kutegemea kushika dola kwa kutegemea madhaifu ya CCM badala uwezo wake kama mbadala.
Amesema  kazi kubwa ya chama chochote cha siasa ni kujiandaa na hatimaye kushinda uchaguzi ili uweze kuunda na kuendesha Serikali na dola kama njia ya maono yaliyo kwenye ilani ya uchaguzi kwa lengo la kuleta maendeleo na ustawi katika nchi.
Masha ambaye aliwani kuwa Mbunge wa Nyamagama mwaka 2005-10,amesema siyo sahihi kwa vyama vya upinzani kuwekeza katika kumpinga Rais Magufuli ambaye ni mkuu wa nchi pekee anayetekeleza kwa vitendo mambo ambayo upinzani ilikuwa ikiyapigia kelele kwa miaka mingi,na kuwashinda viongozi wa CCM  waliomtangulia.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA