MBUNGE MPANDA VIJIJINI:-SERIKALI INA MPANGO GANI WA KUJENGA HOSPITALI ZA WILAYA KATIKA WILAYA MPYA?

Na.Issack Gerald
WIZARA ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) hapa nchini,imeziagiza Halmashauri zote nchini ambazo hazina Hospitali za wilaya kutenga maeneo na kuanza kujenga kulingana na uwezo walionao wakati serikali kuu ikiendelea na Mkakati wa kuoneza nguvu katika ujenzi wa Hosiptali hizo.
Agizo hilo limetolewa leo bungeni Dodoma na Naibu waziri wa Wizara hiyo Joseph Sinkamba Kandege wakati akijibu swali la Mbunge wa Mpanda vijijini Mh.Suleiman Moshi Kakoso aliyetaka kujua mpango wa serikali katika ujenzi wa Hosiptali katika wilaya hususani Mpaya ambazo hazina hosiptali hizo.
Waziri Kandege amesema,serikali katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 imeongeza bajeti na kufikia Zaidi ya Shilingi Bilioni 200 kutoka zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa mwaka wa fedha uliopita.
Mh.Kakoso katika swali lake la nyongeza,amebainisha kuwa kukosekana kwa Hospitali za Wilaya kwa baadhi ya wilaya hapa nchini ikiwemo Wilaya ya Tanganyika iliyopo Mkoani Katavi kunasababisha wananchi kupata adha ya kupata huduma za kiafya.
Wilaya ya Tanganyika ni miongoni mwa Wilaya Mpya zilizoanzishwa miaka miwili iliyopita huku ikikabiliwa na changamoto mbalimbali hasa katika sekta ya maji,afya na miundomboinu ya barabara.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA