WALIMU WANAUSUBIRI MWEZI NOVEMBA KWA HAMU, MADARAJA, MISHAHARA NA MENGINE KEDEKEDE

Na.Issack Gerald-Nsimbo
SERIKALI inatarajia kuanza kulipa madeni,kuajiri na kupandisha madaraja kwa walimu kuanzia mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.

Hatua hiyo imethibitishwa na Mjumbe wa kamati utendaji ya taifa ya chama cha walimu Tanzania CWT Costantine Maricery,ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika leo katika halashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Awali katibu wa chama cha walimu Tanzania CWT Halashauri ya Wilaya ya Nsimbo,Dunstan Mshanga katika risala yake amesema,pamoja na walimu kuidai serikali zaidi ya shilingi milioni 435,pia wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vitendea kazi suala ambalo mgeni rasmi amesema yanafanyiwa kazi.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa chama cha walimu Tanzania CWT Mkoani Katavi Mwl John Gerigori Mshota mbali na kuwataka walimu kuwa na nidhamu mahala pa kazi amesema chama hakitakubaliana na mwajiri atakayemlazimisha mwalimu kufanya kazi nje ya muda unaojulikana kisheria.

Nao baadhi ya walimu wanachama CWT katika Halmashauri ya Nsimbo,wamesema mkutano mkuu umejibu ipasavyo haki za walimu kama inavyotakiwa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA