HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA IMEFUNGUA SEMINA YA USINDIKAJI SAMAKI.

Na.Issack Gerald-Tanganyika
IDARA ya uvuvi Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi imezindua mafunzo ya siku kumi ya uvuvi,uchakataji na usindikaji wa mazao ya samaki.

Afisa  Uvuvi Mkoani Katavi Kayumba Torokoko amesema lengo la kuendesha semina hiyo inayofanyika Tarafa ya Karema Wilayani Tanganyika inalenga kuelimisha wachakataji wengi kujua  namna ya kuhifadhi samaki kwa njia ya kisasa zaidi.
Amesema mafunzo hayo yatakayodumu kwa siku kumi yatapelekea vikundi vingi vya kuchakata samaki kuwa katika ubora mzuri ili kupata soko zuri.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii Tarafa ya Karema Mary Patric Kawogo amesema mafunzo hayo yataongeza uwezo wa wachakataji wa samaki ili ili kuendesha shghuli yenye tija.
Nao baadhi ya washiriki wa semina hiyo wamesema kupitia mafunzo hayo watajua namna  ya kuinua kipato na kuimarika kiuchumi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA