MAJOPKOFU YA KUHIFADHIA MAITI MKOANI RUKWA ZAIDI YA WEZI HAYAFANYI KAZI.

MAJOKOFU ya chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Rukwa yameharibiribika kwa zaidi ya mwezi mmoja mpaka sasa. 

Kaimu Mganga mkuu  wa hospitali ya mkoa wa Rukwa Emanuel Matika,amekiri kuharibika kwa majokofu hayo ambapo amesema wao kama uongozi wametoa taarifa TEMESA lakini kwa kuwa hawanafedha ndiyo maana mpaka sasa hayajatengenezwa.
Kwa mjibu wa Dkt.Matika,utaratibu wa sasa uliowekwa na TEMESA ni lazima walipwe fedha ndipo watengeneze na ambapo wanaendelea na mchakato wa kutafuta fedha ili majokofu yatengenezwe.
Katika hatua nyingine Dk Mtika kutokana na kuharibika kwa majokofu hayo kwa ndugu wanaosafirisha miili ya ndugu zao wanatumia dawa aina ya fomalini ili kuitunza isiharibike. 
Mmoja wa wakazi wa mji wa Sumbawanga Maria Kayanda ambaye mjomba wake alifariki dunia Siku chache zilizopita alisema walilazimika kufanya maziko haraka kutokana na kushindwa kupeleka mwili wa mjomba wake huyo baada ya kupata taarifa kuwa majokofu ya chumba cha kutunzia maiti yameharibika. 
Alisema mjomba wake alifariki usiku na wakafanya maziko siku iliyofuata lakini wao walitamani kuwasubiri ndugu zao wengine waliopo nje ya mji wa Sumbawanga na mkoa wa Rukwa lakini walishindwa na hivyo kulazimika kuzika.
Kutokana na hali hiyo kumeleta usumbufu na gharama kwa baadhi ya ndugu wa marehemu ambao wanapenda kuhifadhi miili ya marehemu ili kuwasubiri ndugu wengine waliombali wafike kwa ajili ya kuhudhuria maziko. 
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA