CWT NSIMBO WAMEFANYA UCHAGUZI WAWAKILISHI MAHALA PA KAZI,NAFASI YA WENYE ULEMAVU KAMA KAWAIDA

Na.Issack Gerald-Katavi
WALIMU wanne akiwemo Onorine Boniface mwakilishi wa walimu wenye ulemavu katika Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi,wamechaguliwa kuwakilisha walimu wenzao katika chama CWT ndani ya halmashauri hiyo wakitoka katika shule wanazofundisha.

Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo Hamis Ismail ambaye ni katibu wa chama cha walimu Tanzania CWT Mkoani Katavi amewataja wengine waliochaguliwa kuwa ni Nelson Mwangole na Amani Shaban kwa upande wa shule za sekondari huku Essa Kyendesya akiwa shule ya msingi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha walimu Tanzania CWT Mkoani Katavi John Mshota ametoa wito kwa waliochaguliwa kuwa wawakilishi kwa kuunganisha walimu kuwa kitu kimoja ili kujenga mshikamano.
Walimu ambao wamechaguliwa wameahidi kufanya kazi kwa bidii kwa kushirikiana na walimu wanachama ili kuhakikisha wajibu,haki na maslahi ya chama yanalindwa kwa manufaa ya chama na taifa.
Wakati huo huo,katibu wa chama cha walimu Tanzania CWT Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo,amesema uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti wa chama cha CWT katika Halmashauri hiyo iliyoachwa wazi baada ya mwenyekiti Kenedy Simsokwe kujiudhuru wadhifa huo itatangazwa baadaye.
Aidha Mw.Mshanga amewataka viongozi 4 wapya waliochaguliwa kutoka shule za sekondari na msingi,kuachia nafasi moja ya uongozi kwa mwenye nafasi zaidi ya mbili huku akiagiza uchaguzi ufanyike kabla ya mwezi Oktoba kukamilika ili kupata viongozi watakaosimamia shughuli za chama katika kituo cha kazi ili kuziba pengo litakalokuwa limepatikana.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA