WAKAZI MJINI MPANDA:KUKATIKA UMEME KERO-Oktoba 4,2017

Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
Baadhi ya Wakazi mjini mpanda Mkoani Katavi wakiwemo wafanyabiasha  wameliomba shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Mkoani Katavi Kuboresha miundombinu yao ili kukomesha tatizo la kukatika umeme mara kwa mara mjini hapa.

Baadhi ya  wakazi hao wakiwemo Prisca Joseph na Wambura Mabula wamesema umeme ndio nyenzo kubwa ya kuendesha shughuli zao hivyo kukatika kwake kunaathiri hali ya kipato kwa kila mmoja.
Katika taarifa yake aliyoitoa hivi karibuni Afisa  uhusiano wa Shirika hilo mkoani Katavi bwana Amoni Michel Bidebuye  amekiri kuwepo changamoto hiyo na kuahidi kuendelea kuzitatua kwa nguvu zote.
Licha ya TANESCO mkoani katavi kuboresha mitambo yao ya kuzalisha umeme, shirika hilo bado halijaweza kufanikiwa kutoa umeme wa uhakika kwa wateja wake.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA