DC MPANDA:SITAMBUI KAMA WANANCHI WANAISHI CHINI YA MITI-Oktoba 4,2017

Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
Baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Mgolokani wakiwa chini ya mwembe kama makazi yao baada ya makazi yao kubomolewa(PICHA NA Issack Gerald)
MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Charles Matinga,amekana kuwa na taarifa kama waliokuwa wakazi wa kitongoji cha Mgolokani kata ya Sitalike Halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo wanaishi chini ya miti kwa tangu Agosti 4,mwaka huu.

Matinga ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu mwafaka wa uhalali wa waliokuwa wakazi wa kitongoji cha Mgolokani wanaodai kuvamiwa na serikali katika makazi yao na kuondolewa kimakosa pamoja na kuharibiwa mali zao.
Aidha matinga amesema kama Halmashauri iliidhinisha wakazi hao kujenga makazi katika kitongoji cha Mgolokani kinachodaiwa kuwa sehemu yam situ wa msaginya ilifanya kosa inatakiwa iwajibike katika tatizo hilo.
Hivi karibuni mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Raphael Kalinga alisema suala hili linashughulikiwa na vyombo vya kisheria ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Nsimbo Mh.Richard Mbogo takribani wiki moja iliyopita aliwataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu wakati wakisubili kurejeshewa maeneo yao mara baada ya vyombo husika kuchukua maamzi.
Wakazi wa kitongoji cha Mgolokani wanadai kuishi katika kitongoji hicho kuanzia mwaka 1974 ambapo mwezi Julai mwaka huu 2017 wahifadhi wa misitu walifika kuhakiki mipaka na wakazi hao kuhakikishiwa kuwa wao wako eneo salama hali ambayo iliwaacha na mshangao nyumba zao zilipoanza kubomolewa.
Zaidi ya kaya 200 zilibomolewa makazi yao kwa madai kuwa walivamia msitu wa hifadhi wa Msaginya na kujenga makazi pamoja na kuendesha shughuhuli za kibinadamu suala ambalo linakanushwa na wananchi hao.
Maeneo mengine yaliyokumbwa na oparesheni ya watu kuondolewa katika makazi yanayodaiwa kuwa sehemu ya hifadhi ya misitu katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ni kaya ya Litapunga na Kitongoji cha Makutanio.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA