DC MPANDA KUSHUGHULIKIA VIBOKO WAVUNJA NDOA ZA WATU NA KUHARIBU MAZAO SHAMBANI-Oktoba 4,2017

Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
MKUU wa wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Matinga amesema atawasiliana na idara ya maliasili pamoja na Shirika la kuhifadhi mbuga za wanyama Tanapa Mkoani Katavi ili kushughulikia malalamiko ya wananchi kuhusu tatizo la viboko wanaotishia maisha ya binadamu na kuharibu mazao shambani kwa wakazi wa kijiji cha milala na maeneo jirani.

Matinga ametoa kauli hiyo leo ambapo amesema pamoja na mambo mengine Ofisi ya Afisa Mtendaji wa kata iandike barua kuelezea tatizo lililopo ili lishghulikiwe haraka iwezekanavyo.
Wiki iliyopita wakazi wa kijiji cha Milala Kata ya Misunkumilo,mitaa ya Kigamboni na Makanyagio, waliilalamikia serikali kutochukua hatua dhidi ya viboko ambao wanaharibu mazao shambani pamoja na kusababisha baadhi ya ndoa kuvunjika kutokana na wanaume kuhamishia makazi yao shambani ili kukabiliana na wanayama hao huku viongozi wa kijiji kupitia kwa afisa mtendaji wa kijiji cha milala Bw.Antipas Kalumbete akisema mara kwa mara wamekuwa wakiandika barua za kuomba msaada lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.
Bwawa la milala ambalo ni miongoni mwa vyanzo vya maji yanayotumika kwa wakazi wa Manispaa ya Mpanda, linasemekana kwa sasa lina viboko zaidi ya tehelathini wanaoharibu mazao shambani na kusababisha wakazi wa maeneo jirani na bwawa hilo kulazimika kujifungia ndani majira ya jioni wakiogopa kushambuliwa.
Katika Mkoa wa Katavi kumekuwa na wanyama pori wakiwemo pia simba kuvamia makazi ya watu na kuleta madhara kwa binadamu ambapo kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Nzyungu amesema kuna ulazima wa hatua kuchukuliwa ni wakazi wake Katika Manispaa ya Mpanda waendelee kuwa salama huku akisem tatizo la viboko limekuwa likijitokeza mara kwa mara.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au Ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA