EQUIP TANZANIA WATOA SHILINGI BILIONI 6 KWA AJILI YA ELIMU KATAVI NA SINDIDA-Oktoba 4,2017

Na.Issack Gerald-Katavi
RC Katavi Meja Jenerali Raphael Muhuga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika makabidhaiano ya mpango huo
Mpango wa kuinua kiwango cha ubora wa elemu katika shule za msingi nchini Tanzania (EQUIP Tanzania) unaotekelzwa na serikali ya uingeeza,umetenga zaidi ya shilling Bilioni 6 kwa mikoa ya Katavi na Singida zitakazotumika kuinua ubora wa elimu.

Haatua hiyo imebainishwa na Bonifasi Joseph ambaye ni Ofisa mkuu wa usimamizi wa fedha EQUIP Tanzania,Katika Mkutano wa kuzindua Mpango huo katika Mkoa wa katavi uliofanyika jana  katika manispaa ya Mpanda na kusema kuwa fedha hizo hupelekwa moja kwa moja katika halmashauri husika.
Amesema Mpango huo unafanya kazi na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI ambapo fedha hizo zinazoletwa Tanzania ni fedha za ruzuku na sio Mkopo.
Mgeni Rasmi Katika Uzinduzi wa Mpango huo Mkoani Katavi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneal Mstaafu Raphael Muhuga amezielekeza halmashauri zote kusimamia fedha hizo kwa umakini na pasijitokeze uzembe au  ubadhirifu wa aina yoyote sambamba na kutoa taarifa kwa wakati na zenye usahihi.
Wakati huo huo Mpango huo utawapatia pikipiki waratibu elimu  kata, kuwafundisha walimu wakuu na walimu wakuu wasaidizi namna ya kutayarisha mipango ya maendeleo ya shule ikiwa pamoja na kupatiwa vishikwambi (Simu kubwa Tableti) ili kuboresha usahihi wa taarifa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mpanda Bi Lilian Charles Matinga amewataka waratibu elimu katika Halmashauri za Nsimbo na Manispaa ya Mpanda zilizo chini yake kuzisimamia fedha hizo ili zitumike kama zinavyotakiwa.
Mratibu Kiongozi wa Mradi wa EQUIP Tanzania Mkoani Katavi amesema Mkoa wa katavi licha ya kufanya vizuri katika elimu ya Msingi Lakini bado kuna baadhi ya changamoto ambazo anaamini mradi huu unazitatua na  kuboresha zaidi kiwango cha elimu Mkoani Katavi
Kwa upande wake Afisa elimu Mkoani Katavi Mwl. Ernest Hinju amesema Kupitia Mradi huu utasaidia kumaliza baadhi ya chanamoto mbalimbali  kama  kuanzisha shule shikizi katika maeneo ambayo hayana shule,Pamoja na kumalizia ujenzi wa madarasa ambayo hayajakamilika.
EQUIP Tanzania Kiutekelezaji Nchini Tanzania umeanza rasmi Mwaka 2014 katika mikoa mitano ya Tabora,Kigoma, Shinyanga,Dodoma pamoja na mkoa wa simiyu na baada ya matokeo mazuri ya utekelezaji wa Mpango huo ikaongezwa Mikoa miwili ambayo ni Lindi na Mara na ulitegemewa kumalizika Mwezi  januari  mwakani lakini tathmini iliyofanyika  kumekua na matokeo mazuri sana ya mpango huo na hivyo kujitokeza fursa ya kuongeza miaka mingine miwili mpango ambao umekwenda samabamba na kuongeza  mikoa mingine miwili ya Katavi na Singida.
Steven Myamba ni kiongozi wa Mpango huo ambaye amepewa jukumu la kusimamia mpango katika mikoa mine ikiwemo ya Katavi na Tabora ili kuhakikisha malengo yanakusudiwa.
Mwandishi:Mdaki Hussein,Mhariri :Issack Gerald

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA