WAJUMBE SAKATA LA MAKINIKIA KUIBUKA NA TUZO LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli leo anatarajia kuwatunuku vyeti wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia na baadaye kufanya mazungumzo na kampuni ya Barrick Gold.

Tanzania na Barrick Gold Corporation zilifikia makubaliano Oktoba 19 mwaka huu na kutiliana saini mkataba wa kutekeleza mwelekeo mpya wa namna kampuni hiyo itakavyoendesha biashara ya madini ya dhahabu yanayochimbwa katika migodi yake hapa nchini,.
Aidha kutiliana saini huko kumekwenda sambamba na na kulipa Dola za Marekani Milioni 300 za kuonesha nia njema ya kufidia madai ya upotevu wa mapato yaliyotokana na biashara hiyo.
Tukio hilo linalotarajiwa kufanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 5:00 asubuhi linatarajiwa kurushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao mbalimbali.

 Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA