UCHAGUZI MWENYEKITI HALMASHAULI YA BUHIGWE MIZENGWE MITUPU-HALMASHAURI IMEZUNGUMZA

Baraza la madiwani wilayani Buhigwe mkoani kigoma, limeshindwa kumchagua mwenyekiti wa halmashauri hiyo, baada ya kikao kilichotakiwa kufanyika kwa ajili ya kumchaguwa mwenyekiti  kuahirishwa kutokana na kutokuzingatiwa kwa taratibu za uchaguzi.

Uchaguzi wa mwenyekiti huyo ulitakiwa kufanyika October 21, ambapo mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Bw.Anoster Nyamoga,alichelewa kufika katika kikao hicho ambapo alifika mnamo saa tisa alasiri badara ya saa nne asubuhi kama mwaliko ulivyokuwa unaeleza , ambapo aliwaomba radhi madiwani hao, na kusema kuwa alikuwa katika majukum mengine ikiwa ni pamoja na vikao vya chama cha mapinduzi.
Kabla ya kikao kufunguliwa Diwani wa viti maalum , tarafa ya manyovu Bi,Eles Gomwa, aliomba mwongozo kwa ajili ya kuahilisha kikao hicho, ambapo aliomba kufanyika kwa vikao vya kuvunja kamati kwanza ,na hatimaye uchaguzi uweze kufanyika, ikiwa ni pamoja na kukamilisha taratibu zingine ambazo zilionekana hazijakamilika katika uchaguzi huo.

Aidha kaimu mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Bw.Wilson Rusibila,alikiri kuwa taratibu za uchaguzi huo haikufuatwa na kuridhia kuahilishwa kwa kkao hicho na kusema kuwa taratibu za kuandaa baraza zitaanza upya ili kuondokana na usumbufu unaoweza kujitokeza katika kikao kingine kitakachopangwa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA