WAWILI WAFARIKI DUNIA KWA AJALI MKOANI RUKWA-Septemba 14,2017

WATU wawili Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa,wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kuanguka.

Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa ACP George Kyando amesem ajali hiyo imetokea juzi ikihusisha gari lenye namba za usajili  T 232 BDG aina ya Howo Mixer lililokuwa likisafirisha zege katika barabara ya Chala Namanyere.
Kamanda amewataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Shabani Supa(31) mkazi wa Tabora na Gaudensia Ernest(33).
Chanzo cha ajali hiyo kimebainika kuwa ni mwendo kasi wa dereva ambapo kamanda Kyando amesema dereva huyo ambaye hajafahamika jina lake amekimbia baada ya ajali hiyo huku juhudi za kumtafuta zikiendelea.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi wa Polisi George Kyando ametoa wito kwa wananchi wote hasa watumiaji wa vyombo vya moto na watumiaji wa barabara kuwa makini na kufuata sheria  na alama za usalama barabarani ili kuzuia ajali.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

0764491096

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA