AKAMTWA NA SILAHA YA KIVITA AINA SMG AKIJIHUSISHA NA UHALIFU NDANI NA NJE YA MKOA WA KATAVI-Septemba 14,2017

Mfano wa silaya aina ya SMG
JESHI la polisi Mkoani Katavi linamshikilia mtu mmoja pamoja na silaha ya kivita aina ya SMG yenye risasi 30 aliyokuwa akiitumia katika uharifu mbalimbali.

Kwa mjibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Kamanda wa polisi mkoani katavi Damas nyanda amesma kuwa mtu huyo ambaye amehifahiwa jina lake kwa sababu za kiupelelezi alikamatwa maeneo ya kibaoni.
Kamanda Nyanda amesema baada ya kumkamata mtuhumiwa alisema silaha imehifadhiwa Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa na hatimaye mke wa mtuhumiwa kuwakabidhi jeshi la polisi silaha aina ya SMG ikiwa na risasi hizo 30 ambapo imeelezwa kuwa silaha hiyo ndiyo iliyokuwa ikitumika katika uharifu wa aina mbalimbali ndani na nje yua mkoa wa Katavi.
Aidha jeshi la polisi Mkoani Katavi limesema linaendelea na oparesheni ya kuwatafuta wahusika wa uhalifu wa ain ambalimbali mkoani Katavi ambapo mpaka sasa wamefikia vijiji 101 ambavyo wamevifanyia oparesheni.
Kufuati tukio hilo kamanda Kamanda Nyanda ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi katika kuibua matukio mbalimbali yanayojitokeza ndani ya jamii ili kuyakomesha.
 Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

0764491096

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA