AUWAWA KWA NGUMI NA MATEKE AKITUHUMIWA KUTOHUDHURIA MSIBA WA KAKA YAKE-Septemba 14,2017

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Frank Mwanarusi(32) mkazi wa katika kijiji cha Ilemba Mjini Laela Mkoani Rukwa,ameuawa na watu sita baada ya kupigwa mateke na ngumi sehemu za ubavu wa kulia na kushoto.

Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa ACP Geroge Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema tukio hilolimetokea juzi majira ya usiku.
Kamanda Kyando amesema chanzo cha mauaji ni ugomvi wa kifamilia wakimtuhumu marehemu kuwa kwa kwanini hakufika kwenye msiba wa kaka yake aliyefariki Septemba 2 mwaka huu.
Kwa mjibu wa Kamanda Kyando,wauaji walimvizia kilabuni na kumkamata na kisha kuanza kumshambulia hadi kufa ambapo hata hivyo mtuhumiwa mmoja amekamatwa na anatarjiwa kufikishwa mahakamani huku juhudi za kuwatafuta waliokimbia zinaendelea.
Wakati huo huo kamanda ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi mkoani humo hukuwakamata watuhumiwa wa mauaji pamoja na wote wanaokuwa najichukulia sheria mkononi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

0764491096

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA