AJALI YA BOTI MKOANI RUKWA,YAUA WENGINE HAWAJAJULIKANA WALIPO-Septemba 14,2017

MTOTO aliyefahamika kwa jina Yakini Said umri wa mwenye miaka miwili amekufa maji na wengine kumi na moja kuokolewa Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa baada ya boti waliyokuwa wakisafiria katika ziwa Tanganyika kupinduka.

Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa George Kyando amesema ajali hiyo ambayo ilitokea jana ikihusisha boti ambayo mpaka sasa haijajulikana jina wala mmiliki wake ilikuwa imebeba abiria kumi na nne ikitokea iktokea kijiji cha kilando wilayani Nkasi ikielekea Kijiji cha Kyala Mkoani  Kigoma ambapo hata hivyo watoto wawili mpaka sasa hawajaonekana na wanahofiwa kuwa huenda nao wamepoteza maisha huku wamiliki ambao nao walikuwa miongoni mwa abiria wakitokomea kusikojulikana.
Hivi punde kabla ya kuingia mitamboni mwenzangu Edward Mganga amezungumza na Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa George Kyando kuhusiana na ajali hiyo.
Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni hali ya hewa ambapo kulikuwa na upepo mkali ziwani uliopelekea hata baadhi ya nyumba kuezuliwa mjini Namanyere Wilayani Nkasi.
Mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa wazazi wake ambao nao walikuwa ni miongoni  mwa abiria kwa ajili ya mazishi.
Wakati huo huo Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa Kamishna Msaidizi wa Polisi George Kyando amewataka wananchi hasa watumiaji wa vyombo vya majini kuwa makini na kiwango cha watu na mizigo inayobeba na kuhakikisha hawazidishi uzito ili kuzuia ajali zisizo na ulazima.
Aidha Pia amewashauri waendesha vyombo hivyo kuzingatie sana suala la hali ya hewa kwa kuwa ndicho chanzo kikubwa cha ajali kama hizo.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA