VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI VYAOMBA UKAMATAJI WATU WENYE ULEMAVU UZINGATIE HALI ZAO WANAPOTUHUMIWA KUFANYA KOSA-Septemba 23,2017

Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
VYOMBO vya ulinzi na usalama Mkoani Katavi vimeombwa kutotumia nguvu kubwa katika kuwakamta watu wenye ulemavu na badala yake watumie wataalamu kwa kujali hali za ulemavu walizonazo.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya watu wenye Ulemavu Mkoani Katavi SHIVYAWATA Bw.Issack Mlela wakati akizungumzia kuhusu ukatiri hasa kwa watoto unaoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Katavi.
Amesema hivi karibuni yupo mtoto mmoja na mwenye ulemavu wa kutosikia(Kiziwi) aliteswa na vyombo vya usalama kwa madai kuwa alikamatwa na nyara za serikali ambapo kwa mjibu wa baadhi ya raia walidai kuwa yupo mwanaume aliyemkabidhi nyara hiyo ambayo ilikuwa nyama pori na kasha kutoweka na hatimaye mtoto huyo akikamatwa na kuendelea kuteswa wakijua kuwa amekataa kuzungumza kwa sababu ya kiburi bila kujua kuwa ni kiziwi.
Kesi ya mtoto huyo imeondolewa mahakamani baada ya asasi za kirai ikiwemo vyama vya watu wenye ulemavu Mkoani Katavi na Ofisi za maendeleo ya jamii kuvalia njuga suala la kukamatwa kwa mtoto huyo aliyekuwa anakadriwa kuwa na miaka 10 wakisema kuwa hana hatia ambapo serikali mahakama iliriridhia hana kosa na mahakama kumwachiwa huru.
Kwa upande wake Kaimu Mratibu wa mradi wa elimu Jumuishi Mkoani Katavi Bw.Stephano Masuluali ametoa wito kwa jamii kuwafichua watoto waliofichwa majumbani ili wapatiwe haki zao kama elimu na mahitaji mengine muhimu kwa kuwa kuendlea kuwaficha majumbani ni kuwafanyia ukatiri.
Kesi kadhaa za watoto kufichwa majumbani na kutopatiwa mahitaji muhimu kama elimu na chakula kama inavyostahili zimekuwa zikiripotiwa katika asasi za kiraia na katika vituo vya polisi mkoani Katavi.

Habari nyingine zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA