RAIS WA ZANZIBAR ATEUA VIONGOZI WA TAASISI MBALIMBALI-Septemba 23,2017

Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi wapya na kufanya mabadiliko katika baadhi ya taasisi mbalimbali za Serikali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana  jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Zanzibar Dk Abdulhamid Yahya Mzee imesema Dk Idris Muslim Hija ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,Joseph Abdalla Meza ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi.
Wengine walioteuliwa ni Juma Ali Juma amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko, Bakari Haji Bakari amekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la  Biashara la Zanzibar na Ali Khamis Juma ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko.
Iddi Haji Makame ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Fedha na Mipango, Kapteni Khatib Khamisi Mwidini ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Unguja na Abeid Juma Ali ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete, Pemba.
Rashid Hadid Rashid ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake, Pemba na Salma Mbarouk Khatib ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni,Pemba.
Uteuzi huo umeanza  Septemba 22,hivyo viongozi hao wanatakiwa kuripoti Ikulu Septemba 24 mwaka huu saa 2:30 asubuhi kwa ajili ya kuapishwa.

 Habari nyingine zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au kupitia P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA