RAIS MAGUFULI ATANGAZA AJIRA 3000 ZA WANAJESHI WAPYA-Septemba 23,2017

Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi Dkt. John Pombe Magufuli, ametangaza kutoa ajira kwa wanajeshi 3000 wapya mwaka huu,ili jeshi la Tanzania liwe na askari wa kutosha.

Rais Magufuli ametoa taarifa hiyo leo alipokuwa akihutubia umma mara baada ya kuwapa kamisheni maafisa wa Jeshi,katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.
Aidha Rais Magufuli katika ajira hizo kutosahaulika  vijana waliohitimu mafunzo ya JKT.
Rais Magufuli leo ametoa kamisheni kwa Maafisa wa Jeshi 422 ambao wamehitimu mafunzo katika chuo cha Monduli,hafla ambayo imekuwa ya kwanza kufanyika katika uwanja wa umma. 

Habari nyingine zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au kupitia P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA