RAIS MAGUFULI AOGOPA KUPOKEA MAJINA YA WAFUNGWA WANAOTAKIWA KUNYONGWA-Septemba 11,2017

Rais John Pombe Magufuli amesema kama rais anaogopa kusaini ili wanyongwe baadhi ya wafungwa ambao wamehukumiwa kunyongwa kutokana na makosa mbalimbali.

Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaama wakati akimuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma na kusema anatambua kuwa idadi wa wafungwa waliohukumiwa kunyongwa ni wengi sasa ila anaomba asipewe hiyo orodha.

"Sisi wanasiasa tunaogopa kunyonga, natambua kuwa sasa orodha ya watu ambao wanatakiwa kunyongwa ni kubwa sana ila mimi naomba hiyo orodha msiniletee kwa sababu najua ugumu wake ulivyo" alisisitiza Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli amesema kuwa amechukua muda mrefu kumteua Jaji Mkuu wa Tanzania kutokana na ukweli kwamba alikuwa anatafuta mtu ambaye anaweza kuendana na dhamira yake ya kupambana na rushwa hivyo alipojilidhisha na jaji huyo ndiyo maana ameamua kumteua kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA