JAJI MKUU MPYA TANZANIA AAPISHWA RASMI-Septemba 11,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemuapisha Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye amemteua kushika wadhifa huo Septemba 10, mwaka huu .

Katika ghafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam iliyohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kitaifa wakiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Majaji wengine wa Tanzania,
Jaji Ibrahim Juma amesema anashukuru kwa kurasimishwa kushika wadhifa huo, ambao amekuwa ana ukaimu takriban miezi nane mpaka alipoteuliwa kuwa Jaji Mkuu.
Katika hotuba yake ya kwanza Jaji Mkuu Ibrahi Juma ameahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa weledi ikiwemo kulinda sheria na kuweka imani kwa wananchi, kwani wao ndiyo watetezi wao.
Ibrahim Juma ameanza kutumikia wadhifa wa Kaimu Jaji Mkuu tokea Januari 18 mwaka 2017, baada ya aliyekuwa Jaji Mkuu wa nchi Mheshimiwa Mohamed Chande Othman kustaafu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA