JUMUIYA YA KUHIFADHI TAMADUNI,MILA NA DESTURI ZA KITANZANIA KANDA YA ZIWA TANGANYIKA YAOMBA KUJENGEWA MAKUMBUSHO-Septemba 11,2017

JUMUIYA ya kuhifadhi,kudumisha na kuendeleza mila na desturi za Tanzania katika ukanda wa ziwa Tanganyika, wameiomba serikali ya awamu ya Tano kusaidia ujenzi wa makumbusho yaliyopangwa kujengwa mkoani Katavi kama walivyoahidiwa na serikali ya awamu ya nne.

Kwa mjibu wa mwenyekiti wa jumuiya hiyo inayojumuisha mikoa ya Rukwa,Katavi na Kigoma Bw.Michael Edward Lusambo ambaye makazi yake yapo hapa Mkoani Katavi,amesema serikali ya awamu ya nne iliwapatia ekari zipatazo 50 katika kijiji cha Ifukutwa Wilayani Tanganyika kwa ajili ya ujenzi wa makumbusho hayo.
Bw.Lusambo amesema ikiwa makumbusho hayo yatajengwa Mkoani Katavi,yatakuwa ya pili hapa nchini baada ya yaliyopo Dar es salaam ambapo miongoni mwa malengo ni pamoja na kuwa na zahanati ya kisasa katika makumbusho hayo.
Kwa upande wake Victory Petro Infinula ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mtemi Beda aliyefariki dunia mwaka uliopita amesema serikali isaidie ujenzi huo kama inavyofanyia kazi mambo mengine yaliyokuwa yamepangwa na serikali zilizotangulia madarakani.
Mkapa sasa kuna waganga kadhaa walio chini ya jumuia hiyo ambapo miongoni mwa ambao wamezungumza na Mpanda Radio Fm katika maeneo yao ya kazi wameeleza kilio chao wakiiomba serikali kuona umuhimu wa suala hilo kama inavyotekeleza mambo mambo mengine yaliyoanzia tangu tawala za serikali zilizopita.
Katika hatua nyingine jumuiya hii ambayo tayari ina usajili wa kutoka serikalini imekuwa ikijihusisha na upandaji miti ya dawa,matunda pamoja na kuhamasisha utunzaji wa vyanzo vya maji mkoani Katavi.
Miongoni mwa makabila yanayotajwa kuwa asilia yanayopatikana kwa wingi mkoani Katavi ni pamoja na Wabende,wapimbwe,wakonongo,waruila na wanyakalema waliopo mwambao wa ziwa Tanganyika.
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa ya Tanzania iliyokuwa na machifu na watemi katika miaka iliyopita ambapo neno Katavi lenye maana ya MZIMU lilibadilika kutoka maneno ya awali Katabhi,Katabi na Mpaka sasa Katavi na sababu ya kubadilika kutokana na baadhi ya watu kushindwa kutamka maneno vizuri.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.co

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA