MJI WA NAMANYERE NKASI KUJENGEWA LAMI KABLA YA 2020-Septemba 11,2017

SERIKALI imesema inatarajia kukamilisha ujezi wa barabara yenye urefu wa kilomita tano kwa kiwango cha lami Mjini Namanyere Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa kama iliyoaihidiwa na serikali wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni Dodoma na Naibu waziri wa Ofisi ya Rais tawala za mikoa na Serikali za mitaa Mh.Suleiman Jafo wakati akijibu swali la mbunge wa Nkansi Kusini Mh.Deuderit Mipata aliyetaka kujua utekelezaji wa ahadi ya rais katika ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami.
Mheshiwa Jafo amesema serikali kupitia wakala wa barabara za mijini na vijijini Tarula anatarajiwa kutekeleza ahadi ya rais kabla ya mwaka 2020.
Wakazi wa mji wa Namanyere ambao ni makao makuu ya Wilaya ya Nkasi wamekuwa wakihangaika kupita katika barabara zilizopo katikati ya mji huo hasa wakati wa masika.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA