MADAKTARI 25 WAGOMEA AJIRA ZA RAIS MAGUFULI-Septemba 6,2017

Madktari 25 kati ya 258 wa Tanzania ambao walikidhi vigezo vya kwenda kufanyakazi Kenya wamekataa ajira zilizotolewa na Rais Magufuli kuwa wafanye kazi hapahapa nchini kutokana na safari yao ya Kenya kuhairishwa.

Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Obadia Nyongole amesema baadhi ya madaktari waliopaswa kuajiriwa nchini wamekwenda kinyume na viapo vya madaktari vinavyowataka kuweka mbele utoaji huduma na sio maslahi kama wanavyofanya wao kwa kuonesha tamaa za kwenda kenya ili kupata mshahara mkubwa.
Dk. Obadia alisema kuwa, madaktari hao 25 wamekataa kuajiriwa na serikali, wakisema kama wangekwenda nje ya nchi basi wangepata malipo mazuri kuliko ambayo watalipwa endapo watakubali kufanya kazi nchini.
Uamuzi wa kuwaajiri madaktari hao 258 nchini Tanzania badala ya Kenya ulitangazwa mwezi Aprili na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu  kutokana na kutetereka kwa makubalino ya serikali ya Tanzania na Kenya kufuatia Mahakama nchini, Kenya kutoondoa pingamizi lililofunguliwa kuhusu ajira za madaktari wa Tanzania nchini humo.
“Rais Magufuli ameamua kuwa, madaktari hao 258 ambao walikuwa tayari kwenda kufanya kazi nchini Kenya waajiriwe serikalini mara moja.”
Mnamo mwezi machi 18, mwaka huu, Rais Magufuli alisema, Tanzania imekubali ombi la kuipa Kenya madaktari 500 watakaoisaidia nchi hiyo kukabiliana na tatizo la uhaba wa madaktari na mgomo wa madaktari nchini humo.
“Matatizo ya Kenya ni matatizo ya Tanzania, tutawapatia madaktari hao 500 ili wakatoe huduma ya matibabu kwa ndugu zetu waliopo Kenya, na kwa kuwa mmenihakikishia kuwa madaktari wangu mtawalipa mishahara inavyotakiwa, mtawapa nyumba za kuishi, na mtahakikisha wanafanya kazi katika mazingira mazuri na salama mimi sina tatizo na naamini mambo yatakwenda vizuri,” alisema Rais Magufuli.
Kwa mujibu wa Dk. Obadia, serikali hutumia kati ya Tsh 60 milioni hadi Tsh 90 milioni kumsomesha daktari mmoja na hutoa ruzuku au mikopo ya bei nafuu kwa watu wanaosomea taaluma ya udaktari kwa tegemeo kuwa baada ya kuhitimu warudi kuja kuhudumia raia waliopo nchini kwao kwalengo la kuisaidia nchi yao.
Agosti 16,mwaka huu serikali kupitia kwa Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Mh.Ummy Mwalimu alisema Mgao wa madaktari hao 258 waliotakiwa kwenda nchini Kenya kufanya kazi,kati yao madaktari 5 walelezwa kuletwa Mkoani Katavi ambapo Manispaa ya Mpanda ilipokea-watumishi 3,Halmashauri ya Nsimbo mtumishi -1 huku mpaka kufika Agosti 16 ya mwaka huu ripoti ya waziri ilionesha mtumishi aliyekuwa amepangiwa Halmashauri ya wilaya ya Mlele alikuwa hajaripoti.
Hata hivyo serikali ilitangaza kuajiri watumishi wa sekta ya Afya 3100 wakiwemo 35 katika Halamshauri tano za Mkoani Katavi kabla ya Septemba 30 mwaka huu.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA