LEO WANAFUNZI WA DARASA LA SABA WANAANZA KUFANYA MTIHANI WA KUHITIMU ELIMU YA MSINGI-Septemba 6,2017

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde
Wanafunzi 917,072 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi leo na kesho (Septemba  7).

Kati ya wanafunzi hao, wavulana ni 432,744 sawa na asilimia 47.19, wakati wasichana ni 484,328 sawa na asilimia 52.81.
Watahiniwa 882,249 watafanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili na 34,823 watatumia lugha ya Kiingereza.
Jumla ya watahiniwa 94 wasioona wamesajiliwa  kufanya mtihani huo, wakiwemo wavulana 58 na wasichana 36.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta),
Dk Charles Msonde amesema maandalizi  yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa vifaa vinavyohitajika katika halmashauri zote nchini.
‘’Dk Msonde amezitaka halmashauri kuhakikisha utaratibu wa uendeshaji wa mitihani unazingatiwa.’’
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA