SERIKALI MKOANI TABORA YATEKETEZA SHAMBA LA MIHOGO YA MWANANCHI-Agosti 17,2017

Mhogo
Serikali ya mkoa wa TABORA imeteketeza shamba la mihogo la mkazi mmoja wa kata ya IPULI mjini TABORA baada ya kushindwa kutii agizo la mkuu wa mkoa wa TABORA la kuondoa mazao yake katika  eneo la Chuo Kikuu cha Askofu Mkuu MIHAYO cha TABORA-AMUCTA.

Akizungumza katika eneo la Chuo Kikuu cha AMUCTA katika kata ya IPULI mjini TABORA,Mwanasheria wa mkoa wa TABORA,Bwana RICHARD LUGOMELA amesema serikali ya mkoa imechukua hatua ya kuteketeza shamba hilo la mihogo  ili kukabidhi eneo hilo kwa chuo kikuu hicho.
Baadhi ya wanafamilia ya JONAS TOSHEMU aliyeodolewa kwenye shamba la mihogo,ESTA YESAYA na ANGELA JONAS wakazi wa eneo la mtaa wa MAILI TANO wamesema hawakupata taarifa za kuondoa mazao yaliyomo ndani ya eneo hilo wanalodai ni mali yao.
Kwa upande wake,Baba wa familia hiyo,Bwana JONAS THOSHEMU amesema wananchi waliokuwa wanaishi katika eneo hilo walilipwa fidia na yeye pia alilipwa shilingi milioni moja na laki tatu.
Amemwomba mkuu wa mkoa wa TABORA,Bwana AGGREY MWANRI kufuatilia masuala matatu aliyoagiza kuangaliwa kabla ya kuchukua hatua ya kusafisha shama lake la mihogo.
Naye msemaji wa  eneo  la AMUCTA,Bwana LUTHER KAWICHE amesema eneo hilo ni lao kwa sababu wana vielelezo vyote na kwa sasa wanataka kuliendeleza eneo hilo.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA