SERIKALI KUJENGA BENKI TANO ZA DAMU SALAMA KATIKA MIKOA MITANO UKIWEMO MKOA WA KATAVI -Agosti 17,2017

Damu salama baada ya uchangiaji Mkoani Katavi(PICHA NA.Issack Gerald)
SERIKALI imesema imepata fedha kwa ajili ya ujenzi wa benki za damu salama katika mikoa mitano hapa nchini ukiwemo Mkoa wa Katavi ili kutatua matatizo ya watanzania yanayotokana na ukosefu wa damu salama inapohitajika kwa wagonjwa.

Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na watoto Mh.Ummy Mwalimu wakati akizungunza na wakazi wa Mpanda Mjini katika viwanja vya polisi ambapo amesema ukosefu wa benki hiyo mkoani Hapa wakazi wengi wanaathirika kwa kukosa damu kwa kuwa bebki ya damu salama kwa sasa ipo Mkoani Tabora.
Wakati huo huo waziri Ummy amesema serikali ipo katika mjadala na wafadhili ili kupata fedha fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya Mkoa wa Katavi ambapo mpaka sasa Mkoa wa Katavi umetenga zaidi ya shilingi bilioni moja ili kuanza ujenzi huo.
Wakati huo huo Waziri Ummy amesema wakati serikali ikiwatetea watumishi wa sekta ya afya kutokana na kufanya majukumu mengi kutokana na uhaba wa watumishi hapa nchni ,serikali imesema haitamvumilia mtumishi yeyote atakayemnyanyasa mgonjwa wakati wa kutoa huduma huku wagonjwa nao wakitakiwa kumtaja mhudumu husika aliyewanyanyasa kuliko kusema sifa ya unyanyasaji kwa watumishi wote hata wasiohusika.
Katika hatua nyingine,Waziri Ummy ametoa wito kwa watanzania kupima afya zao mara kwa mara ili kubaini saratani na magonjwa mbalimbali ambayo yamekuwa tishio na kusababisha vifo vingi vya watanzania ambapo kwa sasa asilimia 80 ya wagonjwa wanaopimwa wanakutwa na saratani ikiwa imefikia katika hatua mbaya.
Waziri anahitimisha leo ziara yake ya siku mbili aliyoianza jana na kufanya ziara katika vituo mbalimbali vya afya mkoani Katavi.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA