JESHI LA POLISI MKOANI KATAVI LAWAPIGA MARUFUKU WAPIGA DEBE KATIKA STENDI ZA MABASI-Agosti 17,2017



JESHI la Polisi kikosi cha usalama barabarani mkoani Katavi,limepiga  marufuku shughuli za upigaji debe katika stendi zote Mkoani Katavi.

Kamanda polisi kikosi cha usalama bara barani mkoa wa katavi John Mfinanga amesema,wananchi wengi wamekua wakipeleka malalamiko juu ya kuwepo kwa baadhi ya wapiga debe kuwepo katika vituo mbalimbali ikiwemo stendi kuu ya mabasi Mpanda.
Aidha Mfinanga amesema jeshi hilo litaendesha oparesheni maalumu katika vituo vyote kwa ajili ya kuwaondosha wapiga debe hao.
Wakati huo huo Mfinanga amesema jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wataendelea kuwachukulia hatua kali wamiliki wa vyombo vya usafiri watakaobainika kwenda kinyume na agizo hilo.
Miongoni mwa malalamiko ambayo yamewasilishwa katika jeshi la polisi kutoka kwa abiria ni pamoja na usumbufu na kuwepo kwa vitendo vya wizi na uporaji wa mali za abiria,vitendo ambavyo vimetajwa kufanywa na baadhi ya watu wanaojulikana kwa jina la wapiga debe.
Hata hivyo siyo mara ya kwanza kwa jeshi la polisi Mkoani Mkoani Katavi kutoa agizo hilo ambapo vitendo hivo vya wapiga debe vimeongezeka hasa baada ya mabasi yanayofanya safari kutoka na kuingia Mpanda kuongezeka kila wakati na hivyo kuwepo kwa ongezeko la vyombo vya usafiri,wapiga debe na abiria.
Kwa sasa Mkoa wa Katavi una mabasi yanayofanya safari zake kutoka Mpanda kuelekea Dar es Salaam,Arusha,Shinyanga,Mwanza,Tabora,Kigoma,Sumbawanga,Mbeya pamoja na safari za ndani ya mkoa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA