BARAZA LA MADIWANI MKOANI MARA LAWAADHIBU WATUMISHI WANNE KWA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA-Agosti 17,2017



Baadhi ya madiwani Mkoani Mara

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya mji wa Tarime mkoani Mara leo Alhamisi, Agosti 17 limewakuta na hatia na kuwachukulia hatua za kisheria watumishi wanne kwa kutumia vibaya madaraka yao na kuisababishia halmashauri hiyo hasara ya mamilioni ya fedha.

Akitoa taarifa ya hatua iliyochukuliwa na kamati ya maadili ya utumishi, mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Hamis Nyanswi amewataja waliochukuliwa hatua hizo kuwa ni Simion Nyadwera aliyekuwa katibu wa idara ya afya ambaye alihamishiwa katika Halmashauri ya Maswa anadaiwa kuchota Sh24 milioni na ametakiwa kurejesha kiasi hicho cha fedha huku Taasisi ya Kuzuia  na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ikitakiwa kumchunguza utumishi wake.
Nyanswi amemtaja mtuhumiwa mwingine kuwa ni Laurenti Marwa aliyekuwa afisa utumishi Mwandamizi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime aliyedaiwa kushirikiana na watumishi 60 kuzisababishia hasara taasisi za fedha na kuiingiza halmashauri hiyo kwenye mgogoro mkubwa.
Amesema kuwa Marwa atapunguziwa mshahara wake kutoka ngazi ya mshahara ya TGTS F yenye kiwango cha mshahara wa Sh1.3 milioni kwenda TGTS E, yenye kiwango cha mshahara wa Sh950,000.
Watumishi wengine ni Sabure Masanja na Quinter Wayoga waliopewa onyo kutokana na makosa yao.
Watumishi hawa hawakuwa tayari kuzungumzia uamuzi uliochukuliwa na baraza la madiwani licha ya kupigiwa simu na kuita bila kupokelewa.
Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko amewataka watumishi wa umma kuzingatia maadili ya kazi zao ili kuwafanya wananchi kupata huduma wanayostahiki badala ya kukutwa na usumbufu usio kuwa wa lazima.




Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA