WILAYA YA UYUI YAANZA KUTOA MIKOPO KWA VIJANA NA WANAWAKE-Julai 19,2017

HALMASHAURI ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora,imeanza kutoa mikopo kwa vikundi vya ujasirimali vya wanawake na vijana katika kata ya Ilolangulu wilayani humo ili kuwasaidia wananchi maskini kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake diwani kata ya Ilolangulu Bw.Mohamedi Linso amesema, kwa sasa  vikundi viwili katika kata hiyo vimekopesheka ambapo vikundi vingine kumi vinatarajia kupewa mkopo huo baada ya kutimiza msharti.

Aidha Bw.Linso ameeleza kuwa lengo la serikali ya awamu ya Tano ni kuwainua  kiuchumi wananchi wenye kipato cha chini kupitia asilimia tano za akina mama na vijana zinazotengwa na kila halmshauri ambapo wananchi wanaotiwa mikopo hiyo wametakiwa kutumia nafasi hizo ili kujipatia maendeleo.

Nao  baadhi ya wananchi waliopatiwa mkopo huo  Frola Robert,Fortunata Philipo na Sikuzan Juma wamesema, mkopo huo utawasaidia kuanzisha biashara mbalimbali ambazo zitawasaidia kujikwamu kiuchumi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ilolangulu Bw.Mussa Hamisi amesema ,viongozi wa serikali ya kijiji hicho bado wanaendelea kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao kuhusu umuhimu wa mikopo inayotolewa na serikali.

Bonyeza P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM kwa habari zaidi

 


 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA