MKUU WA MKOA WA KATAVI MEJA JENERAL MSTAAFU RAFAEL MUHUGA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KIWANDA CHA KUZALISHA MAZIWA MKOANI KATAVI-Julai 19,2017

Katika picha,Wa tatu kutoka Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga akisikiliza maelezo kuhusu kiwanda kutoka kwa mwenyekiti wa Kashaulili Livestock Keepers Bw.Andrea Fumbi(wa pili kutoka kushoto) (Picha na P5tanzania.blogspot.com)
Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga ameweka jiwe la msingi katika kiwanda cha maziwa cha  Kashaulili Livestock Keepers Saccos kinachojengwa katika kata ya Makakanyagio Halmashauli ya  Manispaa Mpanda.
Jiwe la Msingi katika mtaa wa Mpadeco Kata ya Makanyagio kinapojengwa kiwanda cha kuzalisha maziwa
Katika uzinduzizi huo,Mkuu wa  Mkoa ametoa wito  kwa wakazi wa Mkoa  wa Katavi  kujitokeza kwa wingi kuwekeza viwanda ili kujenga Tanzania ya viwanda kama serikali ya awamu ya tano ilivyoagiza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kiwanda hicho chenye wanachama zaidi ya 50 Andrea Fumbi amesema,kiwanda hicho kitagharimu zaidi ya shilingi milioni 600 kwa udhamini wa Benkya TIB,ambapo kinatarajia kuzalisha maziwa ifikapo September mwaka huu.
Wakati huo huo Afisa mazingira Manispaa ya Mpanda Bw.Said Mandua pamoja na mambo mengine amewatoa hofu usalama wa mazingira katika makazi wakazi wa Manispaa ya Mpanda kutokana ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kipo nje kidogo ya mita 60 kutoka chanzo cha mto Mpanda.
Mpaka sasa Mkoa wa Katavi una viwanda viwili vya maziwa ambapo kimoja  kilichopo kata ya Ilembo kilizinduliwa na na mwenge wa uhuru mwezi April mwaka huu.

Bonyeza P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM kwa habari zaidi

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA