KITUO CHA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU MPANDA WAOMBA MSAADA KUKIDHI MAHITAJI YAO MUHIMU-Julai 19,2017

KITUO cha Gethsemani cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu kilichopo kata ya Katumba Halmashauri ya Wilaya Nsimbo Mkoani Katavi,kimeomba mchango wa hali na mali kutoka kwa jamii ili kupata pesa kukidhi mahitaji muhimu ya watoto wanaoishi katika kituo hicho.

Msimamizi wa kituo hicho Bw.Godfred Stephano ametoa ombi hilo leo katika mahojiano na waandishi wa habari.
Aidha Bw.Stephano ameiomba jamii kushirikiana kwa pamoja katika  ujenzi wa mabweni ya wasichana na wavulana ambapo August 8 mwaka huu wanatarajia kuendesha zoezi la uchangishaji ili kupata fedha ya kujengea mabweni hayo.
Hata hivyo,baadhi ya wadau wamekuwa wakijitolea na kuwachangia watoto ambapo Kituo cha Gethsemani mpaka kufikia mwaka jana kilikuwa na watoto zaidi100.
Bonyeza P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM kwa habari zaidi


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA