WAJASIAMALI KATAVI WASEMA KUHAMIA ENEO JIPYA KUMEWAONGEZEA MAPATO,WAIOMBA SERIKALI KUBORESHA HUDUMA MUHIMU KAMA MAJI ENEO LA KAZI-Julai 19,2017

WAJASILIAMALI wanaojihusisha na utengenezaji wa vitu vya thamani vikiwemo Vitanda,kabati na meza waliopo kata ya Misunkumilo  halmashauli ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi,wameiomba serikali kuboresha miundo mbinu katika eneo hilo.

Baadhi wakiwemo Florence Vitalisi na Agness Zacharia ,pamoja na mambo mengine wamesema eneo hilo linakabiliwa na ukosefu wa maji safi na salama kwa ajili ya kunywa na kupikia hali inayowapa ugumu wa kuendesha shughuli za kibiashara.

Kwa upande wake Katibu wa umoja wa wajasilimali wanapasifiki Mkoani Katavi Bw.Jastine Mbahi pamoja na kuipongeza Manispaa ya Mpanda kwa jinsi wanavyowahudumia amesema serikali kutoweka urasmu na badala yake itemize wajibu wake wa kuhamisha makundi mengine ya wajasiliamali wahamie katika eneo lililotengwa kama serikali ilivyofanya kwao ili iwe rahisi kupata wateja na kuinua uchumi wao.

Eneo hilo kwa sasa lina wajasiliamali zaidi ya 400 waliohamishwa kutoka eneo la Pasifiki Kata ya Majengo miezi miwili iliyopita ambapo Ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda ilidai kuwa ni makazi ya watu na hivyo si mahali sahihi kufanyia shughuli za karakana.

Eneo hilo la wajasiliamali ambalo lilizinduliwa na mwenge wa Uhuru mwezi Aprili mwaka huu pia linatakiwa kutumiwa na wenye magari ya kubeba mizigo ambayo hayatakiwi kuwa katikati ya Manispaa.

Bonyeza P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM kwa habari zaidi

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA