WAWILI WAJINYONGA WILAYANI MPANDA KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI



WATU wawili Mkoani Katavi  wamefariki dunia kwa nyakati tofauti kwa kujinyonga.

Tarifa hiyo imetolewa leo  na Kamanda wa Jeshi la Polisi  Mkoa wa Katavi Damas Nyanda,wakati akizungumza na Mpanda radio ofisini kwake juu ya matukio hayo.
Kamanda Nyanda amewataja waliofariki kuwa ni Sumpuli Alikado mkazi wa mtaa wa zamani kata ya kashaulili na Alex Charles mkazi wa Kilimahewa Kata ya Shanwe.
Mpaka sasa chanzo cha vifo hivyo bado hakijulikani na upelelezi unaendelea kufanyika.
Matukio ya watu kujinyonga Wilayani Mpanda na Katavi kwa ujumla yamekuwa yakitokea ikiwemo Wilaya ya Mpanda.
 Mwandishi:Ester Lameck
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA