EKARI 1800 ZAMILIKIWA NA MWANANCHI MMOJA,WANANCHI WAHAHA MAHALI PA KULIMA WAIOMBA SERIKALI WILAYANI TANGANYIKA KUINGILIA KATI.



WANANCHI wa kijiji cha Kamilala  kata ya Katuma tarafa ya Mwese wilayani Tanganyika  mkoani Katavi,wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro wa shamba lililochukuliwa  na mtu moja aliyefahamika kwa jina la Kiyondo zaidi ya ekari 1800 huku wananchi wakiwa hawana maeneo ya kulima .

Wamesema hayo wakati wakizungumza na Mpanda radio kijijini hapo,juu ya mgogoro unaowakabili ambapo wameeleza kuwa   hawana maeneo ya kulima .
Kwa upande wa mwenyekiti wa kijiji cha kamilala Dady Stasheni Songoi amesema  kuwa, Bw.Kiyondo amechukua eneo hilo la wananchi bila kufuata utaratibu.
Kutokana na hatua  hiyo wananchi waliamua kufyeka  shamba hilo jambo ambalo  likamlazimu Kaimu mtendaji ambaye pia ni mkuu wa shule ya msingi  Kayenze Bw.Donatusi Sixmod  kufika eneo la tukio  na kuzungumza na wananchi hao,waliokuwa na hasira kali huku akiwaomba kuwa na subira wakati jitihada zikiendelea kufanyika.
Mwa ndishi:Ester Lameck
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA