WALIMU NA WATENDAJI WA KATA WILAYANI KIBONDO WATAKIWA KUKOMESHA UTORO WA WANAFUNZI


Walimu wa shule za msingi na watendaji wa kata Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma amewataka kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaacha utoro na kuhudhuria shuleni bila kukosa.
Moja ya shule zilizopo wilayani Kibondo Mkoani Kigoma
                                

Wito huo umetolewa na Afisa elimu Shule za msingi Wilayani Kibondo  Bw Joseph Ntirutangwa wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake.
Aidha Bw.Ntirutangwa amesema viongozi wa madhehebu wanatakiwa kutoa wito kwa waumini wao ili kuwahamasisha watoto wao kuhudhuria shule waepukane na kitendo cha kuwafanyisha kazi kwa muda wanaopaswa kuwa shuleni kusoma.
Mara kadhaa wazazi wamekuwa wakilaumiwa uwatumikisha shamani watoto wao na kujikuta watoto hao wanafanya vibaya katika mitihani wanayofanya.
Hata hivyo hali ya ufaulu wa wanafunzi katika Wilaya ya Kibondo siyo nzuri katika takwimu za ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya taifa.
 Mwandishi:Jastin Cosmas=Kibondo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA