MANISPAA YA MPANDA YAANDAMWA ZAIDI NA MAAMBUKIZI YA VVU,KATAVI NAYO NDANI YA MIKOA 10 BORA YENYE VVU NA UKIMWI


Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imeendelea kuwa na maambukizi makubwa ya Virusi vya Ukimwi na kuchangia Mkoa wa Katavi kuendelea kuwa miongoni mwa mikoa 10 ya Tanzania yenye maambukizi hayo.
                                            

Hayo yamebainishwa katika kikao cha Wadu wa kupambana na maambukizi ya VVU na Ukimwi ambacho kimefanyika Manispaa ya Mpanda.
Mratibu wa Ukimwi katika Manispaa ya Mpanda Bi.Mary Byaro amesema kikao hicho kimewakutanisha kujadili mikakati ya kupambana na maambukizi ya Ugonjwa huo katika Manispaa ya Mpanda.
Kikao hicho kimeshirikisha wadau mbalimbali wa kupambana na VVU na Ukimwi wakiwemo Waratibu wa Ukimwi Mkoa wa Katavi,Manispaa ya Mpanda,viongozi wa dini,wazee,vijana na asasi za kiraia ikiwemo SHDEPHA.
Takwimu zinaonyesha kuwa  mwaka 2014,asilimia 6 ya watu waliopima VVU waligundulika na VVU ambao kwa uwiano watu 16 mmoja aligundulika kuwa na maambukizi ya VVU hii ni kwa jinsi zote
Aidha mwaka 2014 maambukizi yanayohusisha wanawake Wajawazito yalikuwa ni  4% ya waliopima VVU kwa uwiano wa watu 23 ambapo katika idadi hiyo mjamzito mmoja alikutwa na maambukizi.
Katika hatua nyingine Takwimu za mwaka 2015 zinaonyesha  waliogundulika na maambukizi kati ya waliopima ni 4% kwa uwiano wa watu 23.
Katika uwiano wa wanawake 21 mmoja alikutwa na maambukizi,kwa uwiano wa wanaume 23 mmoja aligundulikana maambukizi huku wa uwiano wa wajawazito 23 waliopima,mmoja alikutwa na maambukizi.
Wakati huo huo katika mahudhurio ya Kliniki mwaka 2014  takwimu zinaonyesha  28% ya wenza walihudhuria kliniki ya wajawazito na kupima VVU kwa pamoja huku mwaka 2015  47% ya wenza walipima VVU kwa pamoja  na kupelekea ongezeko la hudhurio la wanaume kwenye klininik ya wajawazito
Aidha Takwimu zinaonyesha kuwa watoto waliozaliwa na akina mama wenye VVU  99% walipimwa maambukizi  kwa miaka yote miwili 2014 na 2015 ambapo 6% ya watoto waliopima waligundulika na maambukizi ya VVU
Hata hivyo kwa mjibu wa taarifa ya waratibu wa Ukimwi Manispaa ya Mpanda,changamoto zilizopo katika kupambana na Ukimwi ni pamoja na Ufinyu wa maeneo ya kutolea huduma,Ushiriki mdogo wa wanaume ,Uhaba wa vitendanishi,Ongezeko la watoro wanaotakiwa kupata huduma,Usafiri usio wa uhakika kwenye  shughuli za huduma mkoba,Ukosefu wa kiyoyozi maabara,Wafadhili kuendelea kujitoa kusaidia huduma mbalimbali ikiwemo ununuzi wa madawa  (septrine)  matengenezo ya vifaa  nk
Hata hivyo,licha ya Manispaa ya Mpanda kupambana na changamoto mbalimbali za kukabiliana Ukimwi wameendelea kuweka mikakati ikiwa ni,kuongeza siku za huduma,Kushirikiana na  watoa huduma wa magonjwa majumbani wa taasisi ya (SHIDEFA) ,expert na mama mwam  bata kuwatafuta,Kuongeza vituo vya tiba na matunzo,Ukarabati wa chumba kwa shughuli za maabara ,Bajeti  ya ununuzi wa madawa.
Kwa upande wake Mratibu wa TACAIDS Mkoani Katavi Bw.Yahya Mussa Mumbaga amesema Kiwango cha maambukizi ya VVU katika Mkoa wa Katavi ni asilimia 5.9%,Rukwa asilimia 6.2%,Kigoma asilimia 3.4 na Tabora asilimia 5.1%.
Halikadhalika katika tafiti zilizofanyika mwaka 2011-2012 kiwango cha maambukizi ya VVU kwa wanaume na wanawake wenye umri wa miaka 15-49 nchini Tanzania,Takwimu zinaonesha kuwa kwa ujumla maambukizi kwa Tanzania yamefikia 5.1%,Tanzania bara 5.3% na Tanzania visiwani chini ya 1%.
Maambukizi ya VVU yako juu sana katika mikoa ya Njombe (14.8%), Iringa (9.1%) na Mbeya (9.0%) huku mikoa yenye Maambukizi ya chini ikiwa ni mikoa ya Pemba (0.3%), Unguja (1.2%) na Lindi (2.9%)

Baadhi ya njia kuu zinazopelekea maambukizi ya VVU na Ukimwi Ngono zembe,kushirikiana katika matumizi ya vitu vyenye ncha kali ikiwa miongoni mwao kuna mwenye maambukizi,Ubakaji,kuongezewa damu ya mtu mwenye maambukizi ya VVU,mapenzi ya jinsia moja na kutotumia kinga au mpira ujulikanao kama kondomu wakati wa kujamiana.
Na njia za kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi ni kuepuka hizo njia ambazo zimetajwa kusababisha maambukizi.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA