ZAIDI YA MATUKIO 27 YALIYOTIKISA KATAVI NA NJE YA KATAVI MWEZI MACHI 2016 NA P5 TANZANIA


WATU WATANO WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO YENYE TAMANI YA MIL.60,280,650/= KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI WILAYANI MLELE

Katika tukio la kwanza habari zilizotufikia Machi 4 mwaka huu,Jeshi la Polisi Wilayani Mlele Mkoani Katavi lilimkamata Bw. Robert Nyakie(40) mkazi wa kijiji na Kata ya kanoge barabara ya tatu kwa tuhuma ya kukutwa na meno ya tembo kinyume na sheria.

Kamanda Msaidizi wa Polisi Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed alisema,mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo Machi mosi mwaka huu katika kijiji cha kanoge barabara ya kwanza.
Aidha,ACP Mohamed alisema,Bw.Nyakie akiwa alikamatwa na vipande  vinne vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 11.50 ambavyo thamani yake ni Shilingi milioni Ishirini na saba na laki saba na Elfu hamsini ambapo kamanda alisema ni sawa na tembo mmoja aliyeuawa.
Kamanda Mohamed alisema harakati za kumpeleka mahakamani Mtuhumiwa huyo aliyekuwa amevichimbia vipande hivyo nje karibu na ukuta wa nyumba yake,zilikuwa zikiendelea ili kujibu tuhuma inayomkabili mara baada ya upelelezi kukamilika.
Hata hivyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi anatoa wito kwa wananchi kutojihusisha na shughuli haramu za ujangiri na biashara za nyara za serikali kwani  ni uhalibifu wa rasilimali za taifa letu hasa kwa manufaa ya vizazi vijavyo na pia  amesisitiza hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa kwa wote wasiotii sheria pasipo kushurutishwa.
Katika tukio la pili siku nne tu baada ya tukio hilo la kwanza la Machi 4,harakati za Jeshi la polisi zilizaa matunda tena Machi 8 mwaka 2016 baada ya kuwatia mbaroni watu 4 kwa tuhuma za kukutwa na vipande vitatu vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 11 vyenye thamani ya shilingi milioni 32,530,650/=ambayo ni sawa na tembo 01 aliyeuawa.

Kamanda msaidizi wa Polisi Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Frank Koroneli (25) Adela Alex (23) Moris ezron (34) na Sedekia Shadrack(38) ambao ni wote wakazi wa kijiji cha Nduwi kata ya Katumba Wilayani Mlele.
ACP Mohamed alisema,mnamo tarehe 05.03.2016 maeneo ya Msasani Kijiji cha Nduwi Station Kata ya Katumba,Jeshi la Polisi likiwa katika doria walipata taarifa toka kwa raia wema kuwa katika Kijiji cha Nduwi kuwa kuna wakazi wanajihusisha na shughuli haramu za ujangili ambapo baada ya taarifa hiyo kupokelewa ndipo walipofuatilia na kuweka mtego na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na vielelezo hivyo huku wakiwa wamevificha vipande hivyo kwenye kichaka.

Hata hivyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ametoa wito kwa wananchi kutojihusisha na shughuli haramu za ujangiri na biashara za nyara za serikali kwani  ni uhalibifu wa rasilimali za taifa letu hasa kwa manufaa ya vizazi vijavyo na amesisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa kwa wale wote wasiotii sheria pasipo kushurutishwa.
Suala la watu kukamatwa  na nyara za serikali bado linaendelea kufukuta Mkoani Katavi kwa harakahara utadhani kuwa ni wahusika kutoogopa mkono wa sheria huku inaonekana Msemo za Mwenzako akinyolewa zako tia maji ukiwa umeshindwa kutimia.
Harakati za Mpanda Radio zinaendelea ili kupata ukweli zaidi kujua zaidi wangapi waliokuwa wakiwafanyiwa upelelezi na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali wamefikishwa mahakamani hususani mwezi machi mwaka 2016.
JERA MIAKA 20
Katika hatua nyingine Jumatano ya wiki hii Machi 30 ,mwaka 2016,mahakama  ya wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imemuhukumu mtu mmoja kwenda jera miaka ishilini baada ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na  nyama ya kiboko.
Akisoma hukumu hakimu mkazi mfawizi wa mahakama hiyo Bw Chiganga Twengwa alimtaja mtuhumiwa  kuwa ni Ramadhani Majengo (66) mkazi wa masigo wilaya ya Mlele.
Alisema mnamo Mei 5 mwaka jana,mtuhumiwa  alikamwatwa na jeshi la polisi akiwa  na kilo 40 za nyama hiyo bila kuwa na kibali cha mkurugenzi wa wanyama poli.
Kufuatia hukumu hiyo,mahakama imetoa amri kwa jeshi la polisi kumkamata kwa nguvu  mtuhumiwa kwa sababu  ya kuluka dhamana .
Pia mahakama imetoa hukumu hiyo   kama fundisho na onyo kali kwa watu wenye tabia  ya kuuwa wanyama poli bila kuwa na kibali cha serikali.

KATIKA HABARI ZA WIZI WA WATOTO MKOANI KATAVVVI NA MWANZA HALIKADHALIKA FEDHA KWA NJIA YA  MTANDAO.

WAWILI WILAYANI MPANDA WAKAMATWA WAKITUHUMIWA KUIBA MTOTO  

Na.Vumilia Abel
Tuanzie na hii ya wizi wa watoto,Tukianzia Katavi

Machi 15 mwaka huu,serikali ya kijiji cha Ikaka kata ya Mnyagala Wilayani Mpanda mkoani katavi kiliwakamata watu wawili wanaofahamika kwa majina ya Edefance John na Januari Kisulo wote wakazi wa kijiji cha  Isengule kata ya Ikola  kwa tuhuma za wizi wa mtoto mwenyeumri wa miaka 13.

Taarifa ya kukamatwa kwa wezi hao ilibainishwa Machi 15 na Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bw. Bw.leonard Michael Mbogambi kupitia kikao cha hadhara kilichwashirikisha wananchi kikilenga kujadili kusoma mapato na matumizi ya mradi wa maji.
Aidha mtendaji huyo alikuwa amesema kuwa watu hao waliokamatwa watapelekwa katika vyombo vya sheria na ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo.
Awali mwenyekiti wa kijiji hicho B w.Mipawa Pikipiki alisema kuwa watu hao aliwapokea majira ya saa 4 asubuhi wakiomba hifadhi ya kulala nyumbani kwake ili kesho yake waendelee na safari ambapo hakufahamu kuwa mtoto waliyekuwa naye siyo wao.
Kwa upande wake askari wa sungusungu wa kijiji hicho Bw.Fredy Nkana Tung’ombe ametoa lawama kwa wazazi juu ya tukio kwa kutomtimiza mahitaji muhimu ya mtoto.
Kwa kwa mujibu wa askari huyo, mtoto huyo ambaye hata hawezi kujieleza amekosa mahitaji ya msingi ikiwemo elimu,mavazi na chakula.
Kwa upande wa watuhumiwa,walikana kuiba mtoto ambapo walidai kuwa walifuatwa na mtoto huyo baada ya kumwomba awaoneshe njia ya sehemu wanakoelekea.
Kwa upande mama mzazi wa mtoto huyo Bi.Pascharia Valentino ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kalofesi alisema alikuwa akiishi na watu hao kwa mwezi mmoja mpaka kufikia machi 15 mwaka huu.
Suala la tabia za watu wasiokuwa na haya juu ya wizi wa watoto halikuishia Katavi pekee mwezi huu tuelekee mwanza kuona nako hali ilikuwaje.
WIZI WA MTOTO KUIBIWA MKOANI MWANZA MACHI 26,2016
Albert-Mwanza.
Mwanamke mmoja ambaye hakutambulika maramoja anatafutwa na jeshi la polisi Mkoani Mwanza  kwa tuhuma za kuiba mtoto mchanga katika wodi ya wazazi katika  Hospitali ya wilaya ya Magu na kutoweka naye kusiko julikana.
Tukio hilo limetokea Machi 23 mwaka huu katika Hospitali ya wialaya Magu ambapo mwanamke mmoja ambaye hakutambulika maramoja akiwa amevalia ushingi aliingia ndani ya wodi hiyo na kutoweka na mtoto huyo.
Kamanda wa Polisi Mkao wa Mwanza Justus Kamugisha ameeleza kuwa mwana mke  aliye ibwa mtoto ni Bi Magdarena Petro (16)  na tukio hilo lilitokea akiwa usingizini ikiwa ni siku moja tu baada ya kujifungua na Polisi mkoani humo inawahoji Manesi, wauguzi na walinzi wa hospitali kwa tukio hilo.
Aidha Jeshi la polisi limeitaka jamii kutoa taarifa ya mtu atakaye kuwa ame husika na wizi wa mtoto huyo na akibainika atafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.End’s
Matukio haya ya wizi wa watoto si mara ya kwanza kuripotiwa hapa nchini na hakuna budi suala hili liangaliwe kwa kina likianzia kwa jamii yenyewe kwa ujumla.
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, March 02, 2016

Na.Issack Gerald-Katavi

Katika Mwezi Machi Mwaka huu kuliibuka sakata lililowahusisha wajasiliamali wakiwa katika harakati za kutafuta maslahi baada ya Umoja wa wajasiliamali wa Pasifiki waliopo mtaa wa majengo kata ya Kashaulili  pale umoja huo uliposhuhudiwa ukiilalamikia Manispaa ya Mpanda kwa kutoa tenda ya kutengeneza madawati kwa mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Sailoni Mwagama ambaye ni mjasiliamali wa eneo hilo tofauti na ilivyokuwa awali kuwa wajasiliamali hao wangepata tenda hiyo kwa pamoja kama ilivyokuwa imetangazwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw.Pazza Mwamlima.
Kutokana na kuwa sakata hilo lilianza kufurukuta mwezi Februari,Machi 2 mwaka huu suala hilo lilimbandua Ofisini Mkuu wa Wilaya ya Mpanda na hatimaye kufika eneo hilo la wajasiliamali kusuluhisha mgogoro huo wa kimaslahi.

Akitoa ufafanuzi wa malalamiko hayo Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda,katibu tarafa wa Tarafa ya kashaulili Bw. Reginard Muhango katika mkutano uliofanyika  eneo hilo Machi 2, alifafanua kuwa lengo na hadi ya mkuu wa wilaya ilikuwa ni kutoa tenda kwa kila mwana pasifiki na si kwa mtu mmoja.
Wakati Bw. Mhango akiwatoa wasiwasi wajasiliamali hao pia aliwaahidi kuwa huo siyo mwisho wa tenda kufika mahali hapo.
Hata hivyo katibu tarafa huyo alimuamru mwenyekiti wa umoja huo katika eneo la Pasifiki,kugawa magogo kwa kila mjasiliamali ili kutengeneza madawati hayo.
Aidha alitoa wito kwa wajasiliamali hao kuendelea na kazi kama kawaida pamoja na kudumisha umoja kati yao na kuchangamkia fursa wanazopata ili kutengeneza vitu vyenye ubora na ustadi wa hali ya juu.
Tenda ya utengenezaji wa madawati kwa ajili ya Shule zilizopo Wilayani Mpanda ilitangazwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda mnamo Februari 27 mwaka 2016 ambapo zaidi ya Magogo 130 yalitakiwa kugawanywa kwa wajasiliamali hao zaidi ya 300 badala yake kuchukuliwa na mtu mmoja hali ambayo ndiyo iliyosababisha hali ya kutoelewana kwa wajasiliamali wenyewe na hatimaye Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kulalamikiwa na kulazimika kuingilia kati.
Ukiangalia hapa zilikuwa ni harakati za Manispaa ya Mpanda kuondoa tatizo la wanafunzi kukaa chini kwa kigezo cha kukosa madawati.
Lakini tukisalia katika suala la madawati ambapo tutasema kuwa ni neema kwa kiasi Fulani ni pale Machi 24 mwaka huu,Wadu mbalimbali wa elimu katika Manispaa ya Mpanda na halmashauri ya Wilaya ya Mpanda walipofanya harambee na kupata kiasi cha shilingi miloni 5 na elfu 65,madawati 224,mifuko 10 ya simenti na magogo 4 ya mbao kwea ajili ya kutengeneza madawati.
Akizungumza wakati wa harambee hiyo,mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bw.Pazza Tusamale Mwamlia aliwapongeza wadau hao kwa michango hiyo na kuwaomba kuendelea kuchangia kwa hiari.
Alisema kuwa Jamii haina budi kuendelea kujitolea kuchangia madawati kwani kila suala haliwezi kukamilika kwa kutegemea bajeti ya seriklai pekee.
Alisema kuwa changamoto ya madawati kumetokana na ongezeko kubwa la wanafunzi waliojiandikisha darasa la kwanza mwaka huu ambapo kwa kiwango cha juu baadhi ya shule zimesajili wanafunzi hadi 800 kwa darasa la kwanza pekee.
Mkuu wa Wilaya pamoja na kutoa shukrani kwa wadau waliojitokeza kufanikisha harambee hiyo,pia aliitaka jamii kwa ujumla kuendelea kujitolea akisema kuwa kutegemea pekee bajeti ya serikali haitoshi.
Akisoma taarifa ya hali ya Mahitaji ya madawati katibu wa kamati ya kuratibu na kutengeneza madawati Bw.Lukasi Sotel Nyambala alisema kuwa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda ina upungufu wa madawati 8245 ambapo imetengeneza madawati 1500 huku yanayohitajika kutengezwa yakiwa ni 7250 .
Kwa upande wa Manispaa ya Mpanda Bw.Nyambala alisema kuwa Manispaa ina upungufu wa madawati 5179 ambapo yaliyotengenezwa ni  554 huku yanayohitajika kutengenezwa yakiwa 4625.
Serikali ya Tanzania ilisema matarajio ni ifikapo mwezi juni mwaka 2016 asiwepo mwanafunzi atakayekaa chini kwa kisingizio cha kukosa dawati la kukalia.
Hata hivyo kwa baadhi ya Halmshauri za Mkoa wa Katavi ikiwemo Manispaa katika taarifa ya mapema mwezi Januari kufuatia agizo la serikali kutolewa likiwataka wakurugenzi na viongozi wa ngazi za juu wa Mkoa wakitakiwa kutafuta ufumbuzi wa tatizo la wanafunzi kukaa chini walisema watatoa taarifa ya mafanikio ya utatuzi wa changamoto ya madawati ifikapo Machi 31.Kwa hiyo Maiki zetu zitaelekea katika Ofisi za Halmshauri wakati wowote.
Na Mpaka Machi 30,mwaka 2016 taarifa ya Halmshauri ya Wilaya ya  Mpanda ni kuwa imeazimia  kukamilisha  agizo la serikali juu ya kutatua changamoto ya upungufu wa madawati   ifikapo May 30 mwaka huu.
Taarifa ya mwandishi wetu Agness Mnubi ilibainisha kuwa Kaimu Mkurugezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Kennedy Shilumba inaeleza kuwa wamejipanga kuhakikisha ifikapo may 30 mwaka huu kuhakikisha wanakamilisha changamoto ya  upungufu wa madawati katika shule za msingi na Sekondari huku serikali ikitoa agizo kukamilisha zoezi hilo ifikapo juni 30 mwaka huu kama agizo la serikali kuu inavyoagiza.
Amesema katika kukamilisha zoezi hili wameshilikisha viongozi mbalimbali pamoja na jamii kwa ujumla.
Amefafanua kuwa Mpaka sasa wamesambaza madawati  1250 na mahitaji ni 6287.
Pamoja na kuiomba jamii kuendelea kushiriki katika kuchangia madawati anabainisha zaidi.

Thursday, 3 March 2016
KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA MKOA.
Katika kikao hicho cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Katavi maarufu kama RCC kilichofanyika Machi 3 katika Ukumbi wa Idara ya maji unaomilikiwa na Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda lakini ukiwa katika ardhi ya Manispaa ya Mpanda kililenga zaidi kujadili masuala mbalimbali.
Kupitia kikao hicho kilichomuhusisha Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania wa awamu ya 10 katika Serikali ya awamu ya Nne,Mh.Mizengo Kayanza Peter Pinda,Waziri Mkuu Pinda aliushauri Mkoa wa Katavi kumaliza migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji pia katika maeneo ya makazi na hifadhi ambayo kwa miaka mingi imekuwa historia kwa baadhi ya maeneo.
Alisema migogoro ya ardhi inasababishwa na ongezeko la watu wanaohamia ndani ya mkoa wa Katavi kutoka mikoa mingine nchini ikiwemo Shinyanga bila kufuata maelekezo ya waraka wa serikali wa mwaka 2000.
Aidha Waziri mkuu mstaafu Pianda alishauri mjadala huo upewe nafasi kubwa na kila halmashauri mkoani Katavi itoe mwongozo wa matumizi ya ardhi na kutoa taarifa katika ngazi ya mkoa ili ufumbuzi wa tatizo hilo upatikane.
Kikao hicho kiliwashirikisha wadau mbali mbali wa maendeleo mkoani Katavi wakiwemo wabunge saba wakiwemo watano wanaochaguliwa na wananchi.
Migogoro mingi katika Mkoa wa Katavi imekuwa ikiibuka ikihusisha wakulima na wafugaji,maafisa kuuza kiwanja kwa mtu zaidi ya mmoja na wakulima kuingia katika eneo la hifadhi za mkoa wa Katavi.

Friday, 4 March 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, March 04, 2016

Na.Meshack Ngumba-Katavi
Katika hatua za Wanawake Mkoani Katavi kujinansua na hali ngumu ya kimaisha,Machi 4 mwaka huu walishauriwa kuunda Vikundi ili kupata fursa ya Kupewa  misaada itakayowasaidia Kujikwamua Kimaisha kwa kuanzisha Miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Ushauri huo ulitolewa na Mh,Taska Mbogo Mbunge Viti maalum Mkoa wa Katavi wakati wa uzinduzi wa Vijiwe vya wanawake Katika kata za Uwanja wa ndege,Makanyagio na Nsemulwa.
Katika Uzinduzi huo Mh Mbogo alitoa Kiasi cha shilingi Milioni Moja na nusu kwa vikundi vyote ili Kusaidia Uendeshaji wa Vikundi hivyo.
Wakizungumza baada ya kupokea Msaada huo  baadhi ya akina mama waliohudhuria uzinduzi huo walipongeza juhudi za Mbunge zinazolenga kuwatoa wanawake katika kundi la watu tegemezi katika jamii.
Mkoani Katavi kumekuwepo vikundi mbalimbali vya wanawake wanaojishughulisha na kazi mablimbali ikiwemo utengenezaji wa sabuni,ufumaji wa vitambaa huku wengine wakijishughulisha na ufugaji licha ya kuwa hakuna soko la uhakika wanakoweza kuuzia bidhaa zao.

 

Tuesday, 15 March 2016

Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday, March 15, 2016

Na.Issack Gerald-Mpanda
Machi 15 mwaka huu,Watu wawili wakazi wa kijiji cha Ikaka  kata ya Mnyagala wilayani Mpanda mkoani Katavi,walifikishwa katika mahakama ya mwanzo mjini Mpanda wakikabiliwa na shtaka la wizi wa fedha kwa njia ya simu  ambayo ni mali ya Charles Lubasha mkazi wa Kakese.

Akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu mwandamizi Bw David Mbembela,askari wa jeshi la polisi WP8940 PC Shakira  aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Bw.Emmanuel Makopo (23) na Cosmas Faustene(33) waliotenda kosa hilo Machi 7 mwaka huu majira ya saa kumi jioni.
PC Shakira alisema washtakiwa hao waliiba pesa zenye thamani ya shilingi laki sita na elfu tano kwa kutumia simu mali ya Lubasha.
Na matukio haya hayakukoma ambapo machi 30 mahakama ya Mwanzo Mjini Mpanda imefuta kesi ya wizi wa kuaminiwa iliyokuwa ikimkabili Michael Maduhu (23) Mkazi wa Karema .
Akifuta kesi hiyo Hakimu Mkazi Sylivester Felix Makombe alisema Mtuhumiwa amefutiwa kesi hiyo kutokana na mlalamikaji Hawa Hamis kutohudhuria Mahakamani.
Mshitakiwa alifikishwa Mahakamani hapo kwa kosa la wizi wa kutoaminiwa,ambapo mnamo January, 22, 2016 alipewa fedha shilingi 90,000/=kwa lengo la kumpelekea mama yake mlalamikaji na hatimaye mtuhumiwa akazitumia mwenyewe.


Tuesday, 8 March 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday, March 08, 2016

Na.Issack Gerald-Mpanda
Machi 8 mwaka 2016,wanawake Mkoani Katavi,waliungana na wanawake wengine duniani kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

Katika Wilaya ya Mpanda maadhimisho haya yalifanyika kwa kufanya usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda wakiongozwa na Mbunge wa viti maalum mkoani Katavi Mh.Anna Lupemmbe ili kuwasidia wagonjwa wasiokuwa na uwezo wa kufanya usafi.
Akizungumzia siku ya Wanawake duniani,mbunge huyo alisema wanawake wamepiga hatua kubwa ya kimaendeleo kutokana na kutambua umuhimu na nafasi yao katika jamii
Kwa upande wao wanawake walieleza  kufurahishwa na maadhimisho hayo wakisema kuwa yamewawezesha kutafakari mchango wao katika kuisaidia jamii kimaendeleo.
Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo machi 8 ambapo siku hii hutumika kujadili masula yanayowahusu wanawake ikiwa ni pamoja na kujadili namna ya kutatua changamoto zinazowakabili.
Maadhimisho haya ya mara ya 41 tangu umoja wa mataifa ulipotangaza rasmi kuanza maadhimisho haya mwaka 1975 yanaongozwa na kauli mbiyu ya ‘’50-50 ifikapo 2030,tuongeze jitihada’’.
Wednesday, 9 March 2016
KICHAPO KWA MADAKTARI NA WAUGUZI NA MADAKTARI KUTOKA KWA WAGONJWA NA NDUGU WA WAGONJWA WATIKISA MWEZI MACHI SASA MIKOA YA KATAVI,MWANZA NA MTWARA YAONGOZA.

Mwezi ni mwezi mwaka 2016 ni mwezi ambao umefurika vituko na matukio ya kushangaza yanayohusisha wagonjwa na ndugu wa wagonjwa kuwadunga makonde ya ngumi wauguzi.
Machi 8 mwaka 2016 mkoa wa Katavi ulianza kwa kushangaza umma pale uliposhudia Muuguzi  Katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda akipigwa na Mgonjwa aliyekuwa akimuhudumia huku serikali ikishauliwa Kuimarisha Usalama wa watumishi Katika maeneo yao ya Kazi.

Katika hali hiyo isiyokuwa ya kawaida imezoeleka kusikia wahuduma wa afya Katika vituo mbalimbali hapa nchini wakilalamikiwa na wagonjwa Kwa Kutumia lugha zisizokuwa na staha,lakini safari hii hali imekuwa tofauti  Kufuatia tukio la Mgonjwa Kumpiga ngumi Muuguzi wa zamu aliyekuwa akimuhudumia Kwa Madai ya Muuguzi Kumtaka Mgojnwa huyo alale Kitanda Kimoja na Mgonjwa Mwenzake.
Bi Recho Matinya ambaye ni Muuguzi Katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambaye pia ndiye Mwathirika wa tukio hilo alisema kuwa alipigwa ngumi,ambapo baada ya hali hii ilimlazimu Muuguzi huyu kuiomba serikali Kukomesha matukio ya namna hii Kutotokea tena kwa watumishi wengine  wa umma na pia Katika sekta nyingine.

Maria Komba mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambapo kwa upande wake alilaani Kitendo hicho na kuitaka Serikali  kuangalia namna ya Kulinda haki za wauguzi akisema kuwa mgonjwa huyo aliamka katika kitanda na kumvagaa muuguzi.
Tukio la muuguzi kupigwa ngumi lilitokea ikiwa ni takribani Wiki Moja kupita tangu wabunge wa Viti Maalumu  Mh,Anna Lupembe na Mh Taska Mbogo Kutembelea Hospitali hiyo ili Kujionea Mapungufu yaliyopo lakini hata kabla hawajaingia ndani Kulitokea Mvutano Kuhusu uhalali wa Kufungwa kwa geti la Kuingia Katika hospitali hiyo Muda wote.
Hata hivyo mgonjwa aliyempiga muuguzi alitokomea siku moja baada ya kumchalaza muuguzi na hakujulikana alikoelekea.
Wakti tukio hili likitokea hapa mkoani Katavi,Mkoani Mwanza wauguzi na madaktari katika Hospitali ya Butimba wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza  walilazimika kugoma kutoa huduma kwa saa sita kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 6 mchana mpaka Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana alipoingilia kati suala hilo kwa madai mbalimbali likiwemo madai ya kunyanyaswa na kutishwa na watu wanaofika hospitalini hapo kupata huduma.
Hata hivyo mambo hayajakoma ikiwa ni mwendelezo wa vijimambo vya mwezi machi kati ya Wauguzi/madaktari na wagonjwa wanaowahudumia ambapo Machi 27 wauguzi na madaktari hatika Hospitali ya Rufani Ligula liyopo Mkoani Mtwara  nao pia waligoma kutoa huduma baada ya kudai kuwa mwenzao amepigwa na ndugu wa mgonjwa hadi kuvuliwa nguo.
Tukio la Daktari kupigwa lilitokea majira ya saa 11 asubuhi baada ya mgonjwa aliyetokana na ajali ya pikipiki kulazwa hospitalini hapo tangu Jumamosi ya Machi 26.
Hata hivyo inadaiwa kuwa mgonjwa alimpiga daktari kwa madai ya kuchelesha kutibiwa ambapo kwa upande wa daktari aliyepigwa Dk Sain Dickson alipigwa na mgonjwa alipokuwa amekwenda kumwangalia mgonjwa baada ya kumwandikia vipimo vya X-ray na kusema kuwa mgonjwa alikuwa akipatiwa matibabu.
Mpaka kufikia Machi 28 mwaka huu kufuatia tukio la ndugu wa mgonjwa kumpiga Daktari Mkoani Mtwara, tayari jeshi la Polisi mkoani Mtwara  linawashikilia watu wawili kwa kitendo hicho cha kumpiga mganga wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi.
Hatua ya kukamatwa kwa watu hao wawili kulithibitisha Machi 28 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe akisema kuwa wathumiwa hao wamekamatwa usiku wa kuamkia Machi 28 wakitaka kutoroka kuelekea nje ya nchi nchini huku wengine watatu wakiendelea kusakwa.
Awali wauguzi na Madaktari wa Hospitali hiyo waligoma kufanya kazi hadi hapo watakapohakikishiwa usalama wao ndipo wafanye kazi.
Machi 29,Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alifika Hospitalini hapo na kusuluhisha mgogoro huo huku akiomba Jeshi la Polisi kuongeza usalama kwa watumishi hao wa Afya.
Haya hali kwa sasa iko hivyo katika baadhi ya Hosptali zetu

Friday, 18 March 2016

Posted By:Issack Gerald | At:Friday, March 18, 2016

DAKTARI wa zahanati ya Kapalamsenga wilayani Mpanda, aliyekuwa akituhumiwa na wakazi wa kijiji hicho kusababisha kifo cha  Bi.Anna Kilangi (49) kwa kugoma kumhudumia, alijifungua salama mwanzoni mwezi Machi mwa huu.

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mpanda ,Dk Jovin Mlinda alimtaja daktari huyo kuwa ni Bi.Rehema Munga aliyejifungua mtoto mwenye uzito wa kilo tatu hospitalini hapo Jumapili ya Machi 20,2016.
Siku moja kabla ya kujifungua,askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutoka kambi ya Ikola walilazimika kuilinda nyumba yake baada ya wananchi wenye hasira kutishia kuichoma moto .
Bi Anna Kilangi kabla ya kifo chake, alifikishwa katika zahanati hiyo saa moja usiku kwa matibabu, lakini daktari huyo alikuwa tayari amelala nyumbani kwake, na kutokana na hali ya ujauzito alishindwa kwenda kumhudumia mgonjwa huyo.
Matukio ya madaktari kulalamikiwa kutotoa huduma kama inavyostahiri  kwa wagonjwa yamekuwa yakitokea hata nje ya mkoa wa Katavi ikiwemo Mkoani Mwanza.



Thursday, 10 March 2016
Kituo cha afya cha Mwangaza kinachomilikwa na manispaa ya Mpanda mkoa wa katavi kimekuwa na changamoto mbalimbali  ikiwemo kukosekana kwa vitendea kazi na kupelekea wagonjwa kukosa humuma iliyo bora.

Hayo yalibainishwa machi 10 mwaka huu  na wajumbe wa kamati ya bodi ya manispaa pamoja na wananchi waliohudhuria katika ziara ya mbunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA Bi.Roda Kunchela katika ziara aliyoifanya kituoni hapo.
Walisema kuwa wanahitaji umeme wa ziada ili kuondoa changamoto ya kukosekana kwa  umeme unapokuwa umekatika.
Akijibu na kutolea ufafanuzi  changamoto hizo Mh.Kunchela alisema amesikitishwa na suala la hali ya kituo hicho ambapo alijitolea Sola kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo.
Aidha aliwaahidi kutatua changamoto ambazo zinahitaji utatuzi wa haraka  na kuwataka wafanyakazi kufanya kazi kwa wito ili kuhudumia jamii inayo wazunguka.
Mwezi Machi ni mwezi ambao wabunge na madiwani walikuwa wakifanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi katika maeneo wanayoyatawala huku wananchi wakieleza kero zao ili zipatiwe ufumbuzi kama waheshimiwa walivyoahidi.

Thursday, 10 March 2016
WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

Machi 10 mwaka huu,Kamati ya kulea balaza la watoto wanaoishi katika mazingira magumu yenye mradi ujulikano kama mradi wa elimu Jumuishi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,walikutana na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu.

Kwa mjibu wa Mkurugenzi wa Shirika la IAS Tanzania Bi.Elizabert Mavoa ambaye alifanya ziara mkoani Katavi na kuzungumza na kamati hiyo,alisema lengo la ziara yake ni kupata taarifa mbalimbali ili kufahamu changamoto zinazowakabili watoto wenye mahitaji maalumu katika mikoa ya Rukwa na Katavi.
Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa elimu Jumuishi  Tanzania Bi.Irene Shayo akaiasa kamati kushirikisha jamii na serikali kutatua changamoto za watoto wenye ulemavu.
Naye mratibu wa mradi wa elimu jumuishi katika mikoa ya Rukwa na Katavi Bw. Joseph Ndomba alisema kuwa katika Mkoa wa Rukwa na Katavi tangu kuanzishwa kwa mradi katika mikoa hii mwaka 2012,kuna mafanikio makubwa ikiwemo idadi ya wanafunzi wenye ulemavu kuongezeka shuleni ili kupata elimu kama  watoto wengine wasio walemavu.
Wakati huo huo,katika kuhakikisha kuwa wanatatua changamoto ya vitendea kazi,mradi wa elimu jumuishi ulipatiwa zana mbalimbali ikiwemo gari na vifaa vingine ambapo mradi huu hufanya kazi katika Wilaya za Mpanda,Nkasi na Sumbawanga.
Mradi wa elimu Jumuishi wa awamu ya pili ulianza mwaka 2015 mbapo kila mradi hudumu kwa kipindi cha miaka 3 kabla ya kusaini mkataba wa mradi mwingine.
Mpaka sasa tangu mwaka 2012,mikoa pekee ya Katavi na Rukwa kati ya mikoa 30 ndiyo mikoa iliyopewa kipaumbele kwa mradi wa elimu jumuishi hapa Tanzania.
Mwaka 2015,jumla ya wtoto 62 wenye mahitaji maalumu Wilayani Mpanda waliokuwa hawapewi kipaumbele, waliibuliwa na kupelekwa kati shule mbalimbali kusoma wakiwemo wawili wenye ulemavu wa ngozi Albino walipelekwa kusomea Sumbawanga Rukwa.
Kamati ya balaza la mradi wa elimu jumuishi Wilayani Mpanda,inafanya kazi chini ya ufadhili wa mashirika matatu yaliyoungana na kuunda umoja wao unaojulikana kama IFI.
Mashirika haya  ni International Aids Services(IAS),Free Pentekoste Church Of Tanzania(FPCT) na International Center Of Disabilities
Friday, 11 March 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, March 11, 2016

NA.Issack Gerald-Katavi
Machi 11 mwaka huu,Wafanyabiasha wa soko la Buzogwe wamelalamikia hatua ya kikosi cha zima moto Manispaa ya Mpanda mkoani wa Katavi  kwa kuwatoza kodi ambayo haijulikani inakopelekwa pamoja na kutoelimishwa juu ya michango hiyo.
Wakizungumza katika mkutano ulioitishwa na uongozi wa soko hilo,wamesema kikosi hicho  kinawatoza kodi ya Shilingi Elfu Arobaini.
Walisema kuwa askari hao wamekuwa wakiwapa vitisho vya kuwapeleka mahakamani na kuonesha ubaguzi kwa baadhi ya wafanyabiahara kuhusu kulipa kodi hiyo huku wengine wakiwa hawalipi kabisa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa soko hilo Bw. Ramadhani Karata alikiri askari hao kuwatisha wafanyabiashara na kuwakuzia faini kwa wale ambao hawajalipa licha ya kuwa hawana elimu kuhusu michango hiyo.
Akijibu malalamiko hayo, Mkaguzi Mkuu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa katavi Kamanda Edward Kakwale alisema,kodi hiyo ni ya serikali nzima inayojulikana kama kodi ya ukaguzi zimamoto ambayo hutozwa kwa wafanyabiasha walio na maduka yanayotambulika kisheria.
Aidha Kamanda Kakwale akasema kodi hiyo hulipwa  mara moja kwa mwaka mzima na hupelekwa katika mfuko wa serikali kwa ajili ya majukumu mengine ya kiserikali.
Monday, 14 March 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Monday, March 14, 2016

Na.Issack Gerald
Machi 13 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli Machi 13 alifanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 wakiwemo 13 wapya na 13 waliokuwa katika serikali ya awamu ya nne ya serikali iliyokuwa ikiongozwa na Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
 Katikia Uteuzi huo wamo wanawake watano ambao ni,
Anna Malecela Kilango
Shinyanga
Amina Juma Masenza
Iringa
Halima Omary Dendegu
Mtwara
Dkt. Rehema Nchimbi
Njombe
Chiku Galawa
Songwe(Mkoa mpya)
Wakuu wa Mikoa waliotemwa ni Ludovick Mwananzila (Tabora), Fatuma Mwassa (Geita), Issa Machibya (Kigoma), Mwantumu Mahiza (Tanga), Parseko Kone (Singida) na Abbas Kandoro (Mbeya).
Wengine ni Magalula Saidi Magalula (Rukwa) Rajabu Rutengwe (Morogoro), Dk Ibrahim Msengi (Katavi), Asery Msangi (Mara), Elaston Mbwilo (Simiyu) na Ali Rufunga (Shinyanga).
Katika Uteuzi mpya wa wakuu wa mikoa,umewapa nafasi wanajeshi wanne kuwa wakuu wa mikoa.
Wanajeshi walioteuliwa kuwa Wakuu wa Mikoa wapya ni Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga anayekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita na Meja Jenerali mstaafu, Salum Kijuu anayekwenda Mkoa wa Kagera.
Majenerali wengine ni Meja Jenerali mstaafu, Raphael Muhuga anayekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
Uteuzi wa Majenerali kuwa wakuu wa mikoa ulianza kuzua maswali mengi kwa wananchi kulikoni ambapo Machi 15 wakati wakuu hao wa mikoa wakila kiapo Mh.Rais alitoa ufafanuzi huku akitoa wito kwa viongozi hao wa mikoa ikiwa ni sambamba na wakuu wote wa mikoa kuhakikisha usalama unakuwepo.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli aliwataka wakuu wa Mikoa hao Kuhakikisha wanalinda Usalama wa Mipaka ya nchi na Kuhakikisha kila Mtanzania anafanya kazi huku akiagiza Kukamatwa kwa Vijana wanaocheza Michezo ya pulu wakati wa Kazi badala ya Kufanya kazi.

TUANGAZIE KATIKA SUALA LA MISHAHARA HEWA
Machi 15 Wakati wakila kiapo cha maadili utii na utumishi wa umma,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli alitoa siku kumi na tano kwa Wakurugenzi wa halamshauri zote nchini Kufuta Majina ya Wafanyakazi hewa wanaolipwa Mishaha.
Katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mkoa wa Katavi sasa utakuwa na wakuu wa Mikoa watatu tangu kuidhinishwa kwake rasmi mwaka 2012.
1.Dk.Rajabu Mtumwa Lutengwe
2.Dk.Ibrahim Hamisi Msengi na
3.Jeneral Raphael Mugoya Muhuga wa sasa
Mikoa ya Rukwa,Katavi na Kigoma inapakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa Magharibi,Rwanda na Burundi Upande wa Kaskazini huku Mkoa wa Kagera ukipakana na Rwanda Upande wa Magharibi,Burundi upande wa Kusini na Nchi ya Uganda Upande wa Kaskazini.
Na mara hii tukiangalia matokeo ya Agizo la Mheshimiwa Rais kuhusu watumishi hewa mpaka Machi 30 siku 15 alizokuwa ametoa zikiwa zimekamilika huku wakuu wa mikoa 26 ya Tanzania Bara wakiwa tayari wamekabidhi ripoti za uhakiki wa watumishi hewa katika mikoa yao.
Katika ripoti hiyo inaonesha Mkoa wa Shinyanga kutokuwa na mtumishi hewa yeyote kati ya watumishi hewa zaidi ya 2000 huku mkoa wa Mwanza ukiongoza kwa kuwa na watumishi hewa 334.
Watumishi hao zaidi ya 2,000 wameisababishia serikali hasara zaidi ya Shilingi Bil.4 ,huku baada ya mkoa wa Mwanza kuongoza kwa watumishi hewa mikoa mingine yenye kiwango cha juu ikiwa ni Singida, Kigoma, Pwani, Dodoma, Morogoro na Kilimanjaro.
Ripoti hizo ziliwasilishwa jijini Dar es Salaam jana na Wakuu wa Mikoa hao kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene.
 KATIKA MKOA WA KATAVI
Watumishi hewa waliobainika wako 21 ambapo serikali ya Tanzania katika mkoa wa Katavi Pekee imepata hasara ya Milioni 20.7.

 

Wednesday, 16 March 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, March 16, 2016

Wasichana wapatao 500 wanaodaiwa kufanya biashara ya ukahaba nchini Tanzania pamoja na wateja wao zaidi ya 200 wanashikiliwa na polisi nchini.

Walikamatwa kufuatia msako unaoendelea kukomesha biashara hiyo ambayo haikubaliki kwa mujibu wa sheria nchini humo.
Hii ni idadi kubwa kuwahi kukamatwa katika vita dhidi ya biashara ya ukahaba nchini humo.                           


Wengi walikamatwa maeneo ya Kinondoni, Temeke na Ilala 51.
Kamishna wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema wengi wa majambazi hukimbilia kwa biashara ya ukahaba.
“Kuwakamata na kuwahoji kunasaidia kupata mambo mengi sana kuhusiana na haya (uhalifu), hata madawa ya kulevya pia. Wengi unakuta wanajua watu wanaoyatumia, wengine wanashiriki,” aliambia wanahabari.
Aliwaomba wananchi kuwasiadia maafisa wa polisi katika operesheni hiyo.

 

Thursday, 17 March 2016

Posted By:Issack Gerald | At:Thursday, March 17, 2016

Na.Issack Gerald-Katavi
Oparesheni za kuwataka wanaomiliki silaha kuzihakiki linaendelea ambapo Machi 17 mwaka huu,Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi liliwataka wananchi wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha mara moja silaha hizo katika vituo vya Polisi vilivyopo karibu na makazi yao.

Agizo hilo lilitolewa na Kaimu kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed akisema kuwa jeshi la polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu au kikundi kitakachobainika kumiliki silaha kinyume cha sheria na taratibu za nchi.
Aidha, Kamanda alisema walio na silaha majumbani mwao ambazo zilikuwa zikimilikiwa kihalali na kwa sasa ndugu zao waliokuwa wakimiliki silaha hizo na walikwishafariki dunia wafuate utaratibu kwa kuzisalimisha silaha hizo ambapo suala hili linawahusu pia wazee ambao wamefikisha umri usiowaruhusu kumiliki silaha.
Hata hivyo alisema kuwa ni kosa kisheria wanaomiliki silaha kisheria kuziazimishwa kwa makampuni bina binafisi ya ulinzi ambapo pia aliwataka kuacha tabia hiyo mara moja.
Kamanda Mohamed alisema wananchi wanatakiwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi wanapoona viashiria vyovyote vya uharifu ili vidhibitiwe kabla ya kuleta madhara.

 

WAKAZI WAISHIO MLIMA WA LIAMBA LYAMFIPA WATAKIWA KUHAMA KABLA NGUVU YA JESHI KUTUMIKA.
Na.Issack Gerald-Mlele                                                               
Machi 22,baadhi ya wakazi waliojenga nyumba na kuanza kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo katika mlima wa Liamba Lyamfipa uliopo Wilayani Mlele Mkoani Katavi walipewa wito wa kuhama mara moja sehemu hiyo.

Ujumbe huo uliotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bw.Issa Suleiman Njiku Kupitia kilele cha maadhimisho ya siku ya wiki ya maji yalifofikia kilele chake Machi 22 mwaka huu maadhimisho hayo yakifanyika katika Halmshauri ya Wilaya ya Mpimbwe,ambapo watendaji wa vijiji,kata na wenyeviti wa vijiji waliamriwa kusimamia zoezi la kuwaondoa wakazi hao.
Aidha Njiku aliwataka wananchi kuwa waangarifu katika mlima huo na kutafakari madhara yatakayojitokeza ikiwa mlima huo watauharibu.
Alisema wakazi watakaokaidi kuondoka katika mlima wa liamba Lyamfipa watafuatwa na mkuu wa Wilaya akiwa  na Askari ili kuwatoa kwa nguvu.
Awali katika ufunguzi wa maazimisho ya wiki ya maji duniani,serikali ya Mkoa wa Katavi ilisema kuwa itaendelea kulinda vyanzo vya maji vilivyopo Mkoani Katavi ikiwa ni sambamba na kutafuta namna ya kuendelea kutatua changamoto za baadhi ya wananchi hususani kukosa maji.
Hata hivyo baadhi ya wakazi katika Manispaa ya Mpanda walisema kuwa hawaoni haja ya kuwa na maadhimisho ya wiki ya maji ikiwa mwananchi anaendelea kukosa maji ya kunywa yaliyo safi na salama.
Maadhimisho ya Wiki ya maji duniani huanza kila mwka machi 16 ha kufikia kilele chake machi 22.

HATIMA YAKE
Mpaka naingia katika mitambo ya Mpanda Radio fm taarifa iliyopo ni kuwa wakazi hao wameondoka katika eneo hilo hususani katika vyanzo vya maji Kasansa huku baadhi ya wakazi wakielezwa kutoka Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa hii ikiwa imethibitishwa baada ya Kanali Issa Suleimani Njiku kufanya ziara.


C.W.T YAWAMWAGIA MABATI WALIMU WASTAAFU MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald-Mpanda
CHAMA cha walimu C.W.T Mkoani Katavi kimekabidhi mabati 20 kwa walimu 11 wastaafu kutoka katika halamshauri za Nsimbo na Mpanda kwa kila mmoja kama sehemu ya kutambua mchango wao katika sekta ya elimu.
Akikabidhi mabati hayo Machi 24,2016,mjumbe wa kamati ya C.W.T taifa Bw.Costantine Marisel aliwataka walimu kuendelea kuzingatia maadili ya kazi yao.
Alisemakuwa miongoni mwa tabia zinazotakiwa kuepukika ni pamoja na walimu wa kiume kutofanya mapenzi na watoto wa kike,walimu wa kike kufanya mapenzi na wanafunzi wa kike na walimu kuwachangisha fedha wanafunzi fedha ambazo hazitakiwi kuchangwa kwa kuwa kuna sera ya elimu bure.
Pamoja na mambo mengine,nao baadhi ya walimu waliopata msaada huo walikishukuru chama cha walimu CWT kwa kuwajali huku wakisema kuwa ni vizuri kuzingatia pia usafiri wao kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao.
Hatua hiyo CWT  pia ilipongezwa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wazazi wakisema kuwa hata taasisi nyingine zenye uwezo zifanye hivyo kwa ajili ya kuwasaidia kwa kuwa walitoa mchango mkubwa katika utumishi wao.


WAHITIMU MAFUNZO YA UHIFADHI HIFADHI ZA TAIFA WILAYANI KATAVI
Na.Agness Mnubi-Mlele
                         
Machi 24,wahitimu wa Mafunzo ya Kujengwa uwezo wa uongozi katika uhifadhi wa hifadhi za taifa nchini walitakiwa Kujenga Mahusiano Mazuri na Jamii zinazozunguka hifadhi ili kuwawezesha  kupata taarifa za watu wanaojihusisha na matukio ya ujangili.
Kauli hiyo imetolewa na Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Katavi  Luteni Kanali Alex Ntazi Wakati wa  hafla ya Kufunga Mafunzo hayo iliyofanyika Katika Kituo cha Mafunzo Kilichopo Wilayani Mlele Mkoani hapa.
 Bw.Ntazi aliwataka wahitimu kuepuka vitendo vya rushwa,matumizi mabaya ya silaha,ulevi na utovu wa nidhamu na badala yake walinde rasilimali za taifa.
Aidha alisema wanatakiwa kuwa na mahusiano na watu wanaozunguka maeneo ya hifadhi ili kupatiwa taarifa sahihi za ujangili unaofanywa na waharibifu wa rasilimali za nchi.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi mkuu wa hifadhi za taifa Tanzania Bw.Ntango Mtaiko aliwataka wahitimu kuzingatia nidhamu ya kazi na kupamana na ujangili na kudumisha ushirikiano kati yao wenyewe na ndipo wahushe wengine.
Naye Mkurugenzi utumishi na utawala hifadhi za taifa tanapa Bi.Witness Shoo aliwataka wahitimu kufauata sheria,kanuni,taratibu na maelekezo katika kutekeleza majukumu. 
Awali akisoma taarifa ya kituo cha hifadhi cha mlele kaimu meneja mapori ya akiba Rukwa na Huhafwe Mark Chuwa aliiomba idara ya wanyama pori hifadhi za taiafa na Mkoa wa kuujumla kutatua changamoto zinazokikabili kituo hicho ikiwa ni pamoja na ufinuyu wa bajeti,upungufu wa vitendea kazi,mawasiliano na miundombinu.
Katika risala ya wahitumu iliyosomwa  na mmoja wa wahitimu Bi Angela Nyaki waliahidi kufanya kazi kwa weledi kwa kutumia mafunzo waliyoyapata.
Mafunzo hayo ya wahifadhi yaliyohitimishwa Machi 23,yaligawanyika katika makundi mawili amabpo kundi moja lilianza Februari 01 mwaka huu na kumalizika Februari 16 mwaka huu huku kundi la pili likianza Februari 22 na kuamlizika Machi 23 mwaka huu.

400 WABAINIKA KUWA NA MAAMBUKIZI YA KIFUAKIKUU KATAVI,IMANI ZA USHIRIKINA BADO KIKWAZO.
Na.Issack Gerald-Nsimbo
Machi 24 kila mwaka ni maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa kifuakikuu duniani.Kupitia siku hiyo imegundulika kuwa  Zaidi ya wagonjwa 400 wamegundulika kuwa na maambukizi wa ugonjwa kipindupindu huku wagonjwa hao wakipatiwa matibabu na habari njema ikiwa ni kuwa hakuna mtu aliyefariki kutokona na ugonjwa huo.
Takwimu hiyo iliotolewa na mratibu wa kifuakikuu na ukoma Wilayani Nsimbo Mkoani Katavi Dk.Gabriel Kalumuna kwa niaba ya Daktari wa kikufua kikuu Mkoa wa Katavi ambapo amesema kuwa kati ya idadi ya wagonjwa hao hakuna kifo kichojitokeza na wote walipatiwa matibabu.
Alisema kuwa baadhi ya watu kuendelea kuwa na imani za kishirikina zinachangia kuendelea kuwepo kwa ugonjwa huo kwani watu huchelewa kupatiwa matibabu ambayo hata hakuna malipo yoyote.
Alisema kuwa vituo vinavyotoa huduma ya kupima kifuakikuu katika Wilaya ya Mpanda ni Hospitali ya Wilaya ya Mpanda,Kituo cha Afya Karema,Mwese na Mishamo huku vituo vyote vya afya vikitoa dawa kwa wagonjwa.
Miongoni mwa vituo visivyokuwa na uwezo wa kupima ni pamoja na Ilunde.
Aidha alisema kuwa idadi ya wagonjwa ni wanazidi idadi ya vituo vya afya ambapo aliiomba serikali kuviwezesha vituo vilivyoko mbali view na uwezo wa kupima wagonjwa hususani vijijini ambapo vijiji vingi vipo Halmshauri za Wilaya ya Mlele ,Mpanda Vijiji,Mpimbwe na Nsimbo.
Pamoja na mambo mengine pia alisema kuwa ugonjwa huu husababishwa na aina ya vimelea vijulikanavyo kama MICROBACTERIA CHUBA  ambapo huenea kutoka kwa mtu mwenye maambukizi kwenda kwa mtu mwingine asiye na maambukizi kupitia hewa.
Kuna aina mbili za kifuakikuu cha mapafu ambazo hushambulia vioungo kama mifupa,figo,moyo na viungo vingine mwilini ambapo kwa habari nzuri ugonjwa huu hutibika ikiwa mgonjwa atawahi mapema kuanza matibabu.
Dalili za ugonjwa huu ni kukohoa kuanzia mwezi mmoja na kuendelea,kukosa hamu ya chakula,homa za mara kwa mara makohozi yaliyochanganyika na damu,kupungua uzito na kuhisi kifua kubanwa.
Njia moja wapo ya kupambana na ugonjwa huu ni kujenga nyumba ambayo ina madirisha yanayopitisha hewa ya kutosha na kuwahi mapema katika vituo vya afya kupatiwa matibabu.
Kwa takwimu ya Wizara ya Afya,watu wapatao 12000 hapa Tanzania hufariki dunia kutokana na ugonjwa huu.

HABARI KUHUSU MTO KOGA UNAOTENGANISHA MKOA WA KATAVI NA TABORA
Kufuatia Stendi kuu ya Mabasi Manispaa ya Mpanda kuwa gizani kwa muda mrefu licha taa kuwepo bila mafanikio ya kuwaka ilihali uongozi wa Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya kufika mara kadhaa katika stendi hiyo bila ufumbuzi,Machi 28 Uongozi wa Stendi kuu ya mabasi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,ulipaza sauti umemwomba Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Raphael Muhuga kuingilia kati kutatua changamoto ya kutowaka kwa taa za umeme katika stendi tangu mwaka jana pamoja na wasafiri kukosa mahali pa kujikinga mvua na jua.
Ombi hilo likiwa limetolewa na Mwenyekiti Msaidizi wa Stend Bw. Ramadhani Salm Nkwizu wakati akizungumza na Mpanda Radio Katika stendi hiyo akisema kuwa licha ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda na Mkuu wa Wilaya Mpanda kuahidi kutatua changamoto hiyo tangu mwaka jana,hakuna kilichotekelezeka mpaka sasa.
Kwa upande wake Jailos Kipenye amesema kuwa watu wamehofia kuingiliwa na waharifu pamoja na kuibiwa mali zao kutokana na kutokuwepo kwa mwanga nyakati za usiku.
Suala la barabara kutoka Mpanda Kupitia Tabora ikiwa ni takribani miezi 3 sasa tangu katazo la kutumia barabara hiyo kutumika kutolewa wasafirishaji na wasafiri wanakumbwa na adha ya kutofika Tabora kwa muda mwafaka pamoja  na wasafiri kutumia kiasi kikubwa cha nauli.
Aidha viongozi hao wakamwomba mkuu wa Mkoa kushughulikia tatizo la barabara inayoanzia Mpanda hadi Tabora.
Kufuatia hali ya sintofahamu juu ya hatima ya barabara kutoka Mpanda Kuelekea Inyonga hadi Tabora,Machi 25 mwaka huu,Mkuu wa Mkoa wa Katavi alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa barabara kutoka Mpanda Kuelekea Tabora aliitaka serikali ya Wilaya ya Mlele kuendelea kuzuia magari makubwa yakiwemo ya abiria kutoruhusiwa kupita katika barabara hiyo kwa kuwa msimu wa mvua za masika unaendelea isipokuwa akasema kuwa magari madogo yasiyo ya abiria yanaruhusiwa kupita.
Mto Koga hupokea maji kutoka mito ya Rungwa na Chunya kupitia ziwa Rukwa
Barabara ya kutoka Mpanda Katavi hadi Tabora ilizuiliwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk.Ibrahim Msengi aliyezuia barabara hiyo kutumiwa na vyombo vya usafiri Januari 26 mwaka 2016,kutokana na daraja la mto Koga linalotenganisha Mkoa wa Katavi na Tabora kukatika ambapo jumla ya watu 10 walikufa maji baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji.

TUZO KWA H(W) MPANDA
MPANDA.
Aggy
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpanda imepokea cheti na fedha kiasi cha shilingi  Million mia mbili kumi na nne mia tatu arobaini na sita elfu   kutoka Wizara ya elimu ,sayansi na mafunzo ya ufundi kwa kukidhi   vigezo vya  matokeo ya utendaji kazi wa kila siku.
Akizungumza na Mpanda redio Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpanda ambaye pia ni Afisa Elimu idara ya Msingi Kennedy Shilumba amevitaja  vigezo vilivyozingatiwa katika utoaji wa zawadi hiyo ikiwa ni pamoja na huduma bora kwa walimu,na utendaji mzuri wa kazi.
Amefafanua kuwa wamesubiri kupewa maelekezo ya matumizi ya fedha hizo kutoka Wizara lakini wamedhamilia kuzitumia katika kutatua miundo mbinu na madawati katika shule za msingi na sekondari.
Halmashauri ya Mpanda imekuwa ya tisa kati ya Halmashauri 10 bora  zilizopata zawadi hiyo Kitaifa.

C.W.T KATAVI WAFANYA MAANDAMANO KUDAI MALIMBIKIZO YA MADAI YAO
Na.Issack Gerald-Katavi
MACHI 31,CHAMA cha walimu C.W.T Mkoani Katavi kimefanya maandamano ya amani kushinikiza kulipwa madai ya mishahara yaliyodumu takribani miaka mitatu bila kupatiwa ufumbuzi.
Akizungumza wakati wa maandamano hayo mbelel ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi,mwenyekiti wa wa Chama cha walimu Wilaya ya Mpanda Mwalimu Jumanne Msomba amesema wanachohitaji ni majibu kutoka kwa mwajiri wao namna watakavyolipwa madai yao.
Akizungumza na walimu hao nje ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda,Katibu wa CWT Wilison Msolwa amesema sababu kubwa ambayo imewapelekea waandamane ni kikwazo cha muda mrefu kuhusoiana na madai yao.
Walimu hao wanaokaribia 80 wanaotoka katika shule mbalimbali zilizopo Wilayani Mpanda wameshiriki maandamano hayo.
Hata hivyo mapema asubuhi ya machi 31 mwandishi wetu aliyekuwepo wakati wakiandamana ameripoti kuwa kwa mjibu wa walimu hao wanaounda chama cah C.W.T walisema kila ofisi waliyokuwa wakiingia kupata majibu ya madai waliambiwa hakuna msemaji.
Endelea kufuatilia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM kwa habari za ndani na nje ya Katavi.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA