HALMSHAURI YA WILAYA YA MPANDA WAIBUKA NA TUZO YA CHETI KILICHOAMBATANA NA MIL.214,346,000/=


Na.Issack Gerald-Katavi
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpanda imepokea cheti na fedha kiasi cha shilingi  Million mia mbili kumi na nne mia tatu arobaini na sita elfu   kutoka Wizara ya elimu ,sayansi na mafunzo ya ufundi kwa kukidhi   vigezo vya  matokeo ya utendaji kazi wa kila siku.

Akitolea ufafanuzi kuhusu tuzo hiyo,Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mpanda ambaye pia ni Afisa Elimu idara ya Msingi Kennedy Shilumba amevitaja  vigezo vilivyozingatiwa katika utoaji wa zawadi hiyo ikiwa ni pamoja na huduma bora kwa walimu,na utendaji mzuri wa kazi.
Amefafanua kuwa wamesubiri kupewa maelekezo ya matumizi ya fedha hizo kutoka Wizara lakini wamedhamilia kuzitumia katika kutatua miundo mbinu na madawati katika shule za msingi na sekondari.
Halmashauri ya Mpanda imekuwa ya tisa kati ya Halmashauri 10 bora  zilizopata zawadi hiyo Kitaifa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA