MGOGORO WA ENEO LA UCHIMBAJI MADINI MTAA WAELEKEA PAZURI




Na.Issack Gerald-Mpanda
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima amesema mgogoro wa ardhi katika eneo la machimbo ya kokoto na madini aina ya dhahabu uliopo katika kijiji cha Kampuni  unatafutiwa ufumbuzi.

Amesema hayo machi 31,2016 alipokuwa akijibu hoja kuhusu hatima ya malalamiko ya wakazi wa eneo hilo kuilalamikia serikali kwa madai ya maeneo hayo kuchukuliwa na jeshi.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa ,serikali inafanya jitihada kuhakikisha inamaliza migogoro baina yake na wananchi ili kujenga uwajibikaji wa dhati katika shughuli za maendeleo.
Sanjari na hayo Mwamlima amewataka askari wa wawanyamapori katika hifadhi ya taifa Katavi pamoja na jopo zima la uongozi ndani ya hifadhi hiyo kujichunguza kwanza wao wenyewe kwanza kabla ya kutekeleza adhima ya serikali katika mapambano dhidi ya Ujangiri.
Eneo hilo la wachimbaji lina wachimbaji zaidi ya 200 walioanza kuchimba dhahabu tangu mwaka 1980 ambapo zuio la kutochimba dhahabu katika mlima wa kampuni lilitolewa mapema mwezi Januari mwaka huu na Ofisi ya madini na jeshi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA