WANANCHI WAIOMBA SERIKALI WILAYANI MPANDA KUSAJIRI SHULE WALIYOIANZISHA KWA AJILI YA WATOTO



Na.Vumilia Abel-Mpanda
WANANCHI wa Kijiji cha Ikaka A Kata ya Ikaka Wilayani  Mpanda Mkoani Katavi wameiomba serikali  kusajiri  shule iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi pamoja na kutatua changamoto za kielimu zinazowakabili kijijini hapo.
Wananchi hao wakizungumza na waandishi wa habari,wamesema kuwa watoto wao wanakosa elimu bora kutokana na kutokuwa na shule inayotambulika kwa huduma ya elimu.
Mmoja wa walimu wanaofundisha katika shule hiyo Bw.Magembe Ekingo amesema shule hiyo ina Jumla ya wanafunzi 180 ambapo idadi hiyo inajumuisha wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu.
Amesema shule hiyo yenye miaka mitatu tangu ianzishwe ina walimu 3 wa kujitolea ambao hawatoshi ukilinganisha na idadi ya wanafunzi waliopo shuleni hapo.
Bw Magembe ameongeza kuwa shule hiyo ambayo imejengwa kwa nyasi, ina  choo kimoja  huku wanafunzi wakikalia matofali  jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya elimu kijijini hapo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Ngoko Eliasi amesema serikali ya kijiji hicho imeweka mkakati wa kila kaya kuchangia shilingi elfu 40  kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.
Katika Mkoa wa Katavi kuna maeneo mengi yenye tatizo la watoto kutosoma kutokana na umbali mrefu wa shule.
Maeneo mengine ambayo kwa sasa hayana shule maalumu inayotambulika na serikali kwa ajili ya watoto kusoma ni pamoja na Kijiji cha Luhafwe kilichopo Kata ya Mpanda Ndogo iliyopo Wilayani Mpanda ambapo eneo hilo ndilo lililoathiriwa na Oparesheni Tokomeza ujangili mwaka 2013 ikisemekana kuwa eneo hilo ni hifadhi.
Baadhi ya athari zilizojitokeza kipindi hicho ni madai ya wananchi kuwa walibakwa,kuchomewa nyumba ambapo suala hilo lilipelekwa mahakamani kwa usuluhishi.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA