WAKUU WAPYA WA MIKOA WAAPISHWA,HOTUBA YA RAIS MAGUFULI KITANZI KWAO


Na.Issack Gerald
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ametoa siku kumi na tano kwa Wakurugenzi wa halamshauri zote nchini Kufuta Majina ya Wafanyakazi hewa wanaolipwa Mishaha.
                                           
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga kuwa mkuu wa mkoa wa Katavi,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati akiwaapisha wakuu wa Mikoa Wapya 26 wa Tanzania bara aliowateua siku ya jumapili.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewataka wakuu wa Mikoa hao Kuhakikisha wanalinda Usalama wa Mipaka ya nchi na Kuhakikisha kila Mtanzania anafanya kazi huku akiagiza Kukamatwa kwa Vijana wanaocheza Michezo ya pulu wakati wa Kazi badala ya Kufanya kazi.
Miongoni mwa wakuu wa Mikoa walioapishwa mbele leo ni Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Meja Jenerali  Mstaafu Raphael Muhuga anayechukua nafasi ya Dr Ibrahim Msengi.
Rais Magufuli akifafanua sababu za kuweka wakuu wa mikoa wanajeshi katika mikoa ya Rukwa,Katavi,Kigoma na Kagera amesema kuwa ni mkakati wa kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unakuwepo zaidi ikizingatiwa kuwa ni mikoa iliyopo mpakani mwa nchi jirani.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA