WAWILI WAJERUHIWA,YUMO MAMA ALIYEJERUHIWA KWA KUCOMWA KISU KWENYE TITI.


Na.Issack Gerald-Mpanda
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Zuhura Salum(34), mkazi wa Majengo alijeruliwa kwa kuchomwa na kisu kwenye titi la kulia na Iddy Saleh(24), mkazi wa majengo na kumsababishia maumivu makali.

Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29.01.2016 majira ya saa tatu asubuhi katika maeneo ya Majengo “B” Kata na Tarafa ya Kashaulili Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.
Kamanda Kidavashari amesema kuwa mhanga na mtuhumiwa walikuwa wamelala kwenye nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la maridadi ndipo mtuhumiwa aliamka na kumvizi akiwa usingizini na kumchoma na kisu kwenye titi la kulia.
Chanzo cha tukio hili bado kujulikana ambapo hata hivyo mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na anatarajiwa kufikishwa mahakmani kujibu tuhuma inayomkabili.
Wakati huo huo katika tukio lingine mtu mwingine aliyejulikana kwa jina la Kalekwa Otto(28), mkazi wa kamukuswe alijeruliwa kwa kukatwa na panga mkono wa kulia na kwa kushoto na Manyara Otto na kumsababishia majeraha
Aidha Kamanda Kidavashari amesema kuwa tukio hili limetokea juzi 01.02.2016 majira ya saa moja kijiji cha  kamkuswe kata na tarafa ya mwese wilayani mpanda mkoani katavi.
Amesema kuwa mtuhumiwa na mhanga ni mtu na kaka yake ambapo Siku ya tukio wakiwa kwenye kilabu cha pombe huku wakiendelea kunywa ndipo ulipozuka ugomvi kati ya ndugu hawa wawili na Manyara Otto alipomkata kwa panga na mara baada ya kutenda kosa hilo alitokomea kusikojulikana.
Hata hivyo Chanzo cha tukio hili ni ugomvi wa kifamilia kati ya ndugu hawa wawili na Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka alipokimbilia mtuhumiwa ili kujibu tuhuma inayomkabili.   
Wakati huo huo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi amewataka wananchi kujenga mazoea ya kuwasilisha matatizo yao katika mamlaka za kisheria ili yaweze kupatiwa ufumbuzi na badala yake waachane na tabia ya kujichukulia sheria mikononi kwa kufanya vitendo viovu vinavyopelekea matatizo makubwa ndani ya familia.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA