MBUNGE JIMBO LA MPANDA MJINI ATAKA UJENZI CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA KATAVI UKAMILIKE


Na.Issack Gerald-Dodoma
Mbunge wa Mpanda Mjini Mheshimiwa Sebastian Kapufi ameiomba Serikali kuweka nguvu yake katika ujenzi wa chuo kikuu cha kilimo kinachotarajiwa Mjini Mpanda kwa ajiri ya Kuongeza ajira kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi na Mioko mingine.
                                                      
Bungeni Dodoma

                                                
Mbunge wa Mpanda Mjini Mheshimiwa Sebastian Kapufi akiwa na watoto katika Familia yake kabla ya kwenda bungeni wiki iliyopita


Mheshimiwa Sebastian Kapufi ameuliza swali hilo akiwa bungeni Mjini Dodoma ambapoa akijibu swali hilo,Naibu waziri wa Elimu, sayansi,teknolojia na ufundi Injinia Stela Martin Manyanya amesemakuwa tayari tume ya vyuo viku ilikwishatoa hati kwa ajiri ya ujenzi wa chuo kikuu hicho kinachomilikiwa na  Manispaa ya Mpanda ambapo amesemakuwa serikali itaendelea kutoa ushauri wa kitaalamu nakiufundi ili kukamilisha ujenzi wa Chuo kikuu cha kilimo cha Katavi.
Aidha Serikali kupitia wizara ya Elimu, sayansi,teknolojia na ufundi imeshauri Manispaaya Mpanda kushirikisha balaza la madiwani ili kuondoa hali ya sintofahamu juu ya ujenzi wa chuo hicho ambacho kama kingekuwa kinaendelea kujengwa mpaka sasa kingekuwa kimekwishapata Doala za kimarekani Milioni 2.5 kwa udhamini wa benki ya biashara ya AFRICAN TRADING INSURANCE AGENCE.
Hata hivyo Injini Stela Manyanya amesema Manispaa ilikwishapata eneo la ekari 500 kwa ajiri ya ujenzi wa ujenzi wa chuo hicho.
Kwa upande wake Waziri wa elimu sayansi,teknolojia na ufundi Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa chuo hiki kinajengwa na Manispaa baada ya kuomba wizarani juu ya ujenzi wa chio hicho.
Uamuzi wa Ujenzi wa Chuo kikuu cha Kilimo ulitolewa mwaka feb 11,2011 kupitia vikao vya kisheria vya Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda kwa kuzingatia sheria ya seriklai za mitaa serikali ya mtaa no.8 ya 1982(5) kifungu  53 na 54 1(a) na (b) na 2 (b) na (c).
Tume ya vyuo vikuu ilitoa hati ya usajiri wa awali ya uanzishwaji wa chuo hiki  kwa barua yenye kumbukumbu no.TCU/A/40/1A/V34 YA 31/01/2012 ambapo Manispaa ya Mpanda ilikuwa kikishirikiana wadau mbalimbali kikiwemo chuo cha kilimo cha Uingereza kukamilisha masharti ya uanzishwaji wa chuo hiki.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA