WAZIRI MKUU AELEZA AFURAHISHWA NA HALI YA CHAKULA MKOANI RUVUMA


Na.Issack Gerald.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefurahishwa na hali ya chakula mkoani Ruvuma, ikiwa kati ya mikoa inayotegemewa kwa uzalishaji wa chakula kwa wingi nchini.
                                                   
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary   (kushoto kwake )  wakielekea kwenye Chumba cha mapumziko baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songea na kupokelewa na wanachi na viongozi wa mkoa huo Januari 3, 2016.  Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma , Thabiti Mwambungu na kushoto ni Mbunge wa Songea Leonidas Gama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali jana jioni (Jumapili, Januari 3, 2016) katika ukumbi uliopo Ikulu ndogo Songea, Waziri Mkuu  ameutaka  uongozi wa mkoa kuhakikisha kuna  upatikanaji wa masoko kwa mazao mbalimbali pamoja na kuendelea kutoa msukumo kwa wananchi.
Pia, amewapongeza viongozi wa mkoa huo kwa kutoa msukumo kwa wananchi na kufanyakazi, na kusema ni jambo linalosaidia kupanda kwa pato la mtu mmoja  mmoja, hata hivyo hakusita kuwashukuru kwa mapokezi makubwa aliyopata.
“Nawapongeza sana wana Ruvuma kwa kuongeza pato la ndani kutoka kutoka shilingi 654,227, hadi kufikia shilingi 1,800,000 kwa kipindi cha mika 4 tuendelee kujiweka vizuri kwa kuongeza pato la mtu mmoja mmoja” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu Majaliwa pia amesisitiza  kilimo cha umwagiliaji katika maeneo yote yenye mabonde ili wakulima waweze kuvuna bila kutegemea sana kipindi cha masika. Amesema ni lazima kuimarisha huduma muhimu na kusisitiza matumizi mazuri ya fedha zinazopatikana  katika mazao hayo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu amesema  zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wa Ruvuma hutegemea kilimo cha mazao  mbalimbali ya chakula na biashara  yakiwemo mahindi, mpunga ambao unalimwa sehemu za Tunduru na Songea vijijini, korosho  ambazo zinalimwa sehemu za Tunduru, Namtumbo, Nyasa, Mbinga na Songea vijijini na tumbaku  maeneo ya Namtumbo,Mbinga na Songea vijijini.
Alisema, Ruvuma imekua ikizalisha chakula kwa kiwango cha utoshelezi na ziada kwa kipindi cha mwaka 2012 - 2013, 2013 - 2014 hali hiyo imeendelea kuwa nzuri hadi kipindi cha mwaka 2015 - 2016. Mahitaji yakiwa ni tani 469,172 na ziada ikiwa tani 1,950,111, ametaja baadhi ya sababu za ongezeko hilo la tani  ni pamoja na matumizi ya dhana  bora za kilimo, matumizi ya pembejeo za kisasa na urahisi wa upatikanaji wa pembejeo, aliongeza Mkuu wa Mkoa.
Waziri Mkuu Majaliwa ambaye jana (Jumapili, Januari 3, 2016) ameanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma, kesho  siku ya jumatatu  atakuwa na shughuli za kufungua  tawi la Benki ya Posta mjini Songea, kukagua  maghala ya Wakala wa Taifa wa  Hifadhi ya chakula  (NFRA) kanda ya Songea na kukagua  Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Kupitia ziara hii Serikali ina lengo la kuona hali halisi ya utendaji wa shughuli za maendeleo kutoka kwa watendaji mbalimbali, kuwatia moyo na kuweka msisitizo  katika maeneo yaliyopewa kipaumbele hasa katika sekta ya Afya.
Asante kwa kuendelea kuwa namii,endelea kuhabarika na P5 TANZANIA
Chanzo cha habari :Ofisi ya mawasiliano ya Waziri

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA